Home LOCAL DC.BASILLA AAGIZA KUKAMATWA NA KUWEKWA NDANI KWA WAKUU WA IDARA MBILI WILAYANI...

DC.BASILLA AAGIZA KUKAMATWA NA KUWEKWA NDANI KWA WAKUU WA IDARA MBILI WILAYANI KOROGWE

Na: MAWANDISHI WETU, KOROGWE.

MKUU wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi, ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa wakuu wa idara mbili ambao ni  idara ya mipango na takwimu akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya manunuzi Yasin Msangi na mkuu wa idara ya manunuzi ambaye ni katibu wa kamati ya manunuzi Gregory Matandiko, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za serikali kukiuka taratibu za manunuzi katika miradi hiyo.

Uwamuzi huo umetokana na ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi aliyoifanya siku Jumatano Agost 25, akiambatana na kamati ya usalama ya wilaya katika miradi ya ujenzi wa jengo la utawala na Hospitali ya wilaya Makuyuni.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Mhe Basilla amesema katika dhiara hiyo hakuridhishwa na ujenzi wa wodi tatu unafanyika katika eneo hilo, na usimamizi wa miradi mingine hivyo baada ya kukaa kikao cha ndani na kamati ya usalama wilaya, kamati zote za 

ujenzi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Korogwe, wakafikia uwamuzi wa kuwa kamata wakuu wa idara hizo.

“Kaika dhiara niliyofanya nimegundua changamoto zinazosababisha kukwamisha miradi kutokamilika ni baadhi ya watendaji ,nimeagiza kukamatwa kwa wakuu wa idara husika pia nimemuagiza Mkurugenzi wa Wilaya kuvunja kamati zote na kuteua wajumbe wapya katika idara hizo,” anasema Mhe. Basilla.

Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Wilaya ameagiza kusimama kwa shughuli zote za ujenzi wa miradi hiyo kwa kipindi cha siku 14 ili kujiridhisha na matumizi ya fedha zilizotumika hadi sasa katika miradi hiyo.oo

Aidha Mhe. Basilla Mwanukuzi  amemuagiza Kamanda wa Takukuru, kuanza kufanya uchunguzi wa swala hilo kunusuru fedha za serikali zinazoibwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here