WAZIRI wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki liberata Mulamula (wa pili kulia) mara baada ya kumaliza ziara yake katika Banda hilo. |
Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki liberata Mulamula emetoa maelekezo kwa Shirika la Madini nchini STAMICO kujitangaza zaidi ili watanzania na wadau mbalimbali waweze kunufaika na mradi huo wa makaa mbadala makaa ya mawe.
Amesema niwakati mzuri Kwa Shirika la Stamico kujipanga hususani kupitia maonyesho hayo ili Wananchi wajuwe rasimali ambazo zipo katika nchi yao hasa Kwa kupitia wizara ya Madini chini ya Stamico.
Waziri Mulamula ameyasema hayo leo kwenye maonyesho ya 45 ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba Wilayani Temeke ambalo wamepongeza mradi wa mkaa mbala wa makaa ya mawe ambao unazalishwa kwenye mgodi wa kiwila Uliochini ya Shirika hilo
Amesema kuwa amependa bidhaa hiyo ya mkaa aa makaa ya mawe kuhalakisha kwani hata yeye kwenye eneo lake wanahitaji bidhaa hiyo Kwa ajijili ya matumizi ya majumbani.,
“Harakisheni bidhaa hii ili iweze kutumika Kwa Wananchi kwani wanahamu ya kuitimua na kama nilivyosema awali kwamba bidhaa hii hata kwetu Mkoani Kagera Wananchi wanahitaji sana.” Amesema Waziri Mulamula
Ameongeza kuwa amefurahishwa na muonekane wa Banda la Shirika hilo ukilinganisha na nyakati zingine zote na hiyo anaonyesha namna gani wamejipanga hususani katika maonyesho ya Mwaka huu.
Kwaupande wake Ofisa Uhusiano wa Shirika hilo Bibiana Ndumbaro akizungumzia ujio huo wa Waziri wa mambo ya nje Mulamula amesema kuwa ameshukuru Kwa ujio wa Waziri huyo na kuwapa moyo Kwa ubunifu ambao amruona .
Pia ametoa Maelekezo Kwa Shirika hilo kuongeza kadi ya kutangaza mradi huo ili ufike mbali zaidi na watu wauelewe zaidi mradi wa makaa mbadala ambao ukikamilika utaleta tija sana Kwa Wananchi wa Tanzania na nje ya nchi.
Mwisho.