|
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Askofu Simon Chibuga Masondole kwa kupewa daraja takatifu la uaskofu na kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda, katika viwanja vya Kanisa Kuu la Bunda, Mkoani Mara, Julai 4, 2021 |
|
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia waamini wa Jimbo Katoliki Bunda, baada ya kusimikwa kua Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda, Simon Chibuga Masondole kwa kupewa daraja takatifu la uaskofu na kusimikwa kuwa askofu wa jimbo Katoliki Bunda, katika viwanja vya Kanisa Kuu la Bunda, Mkoani Mara, Julai 4, 2021 |
|
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande akimkabidhi Bakora ya Kichungaji, Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda, Simon Chibuga Masondole kama alama ya kazi ya uchungaji, wakati wa tukio la kupewa daraja takatifu la uaskofu na kusimikwa kuwa askofu wa jimbo Katoliki Bunda, katika viwanja vya Kanisa Kuu la Bunda, Mkoani Mara, Julai 4, 2021 |
|
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande akimvisha Mitra Askofu Simon Chibuga Masondole, wakati akimpa daraja takatifu la uaskofu na kumsimika kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda katika viwanja vya Kanisa Kuu la Bunda, Mkoani Mara, Julai 4, 2021 |
|
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande akiwa ameweka kitabu cha injili kichwani mwa Askofu mteule wa Jimbo Katoliki Bunda Simon Chibuga Masondole wakati wa tukio la kupewa daraja takatifu la uaskofu na kusimikwa kuwa askofu wa jimbo Katoliki Bunda, katika viwanja vya Kanisa Kuu la Bunda, Mkoani Mara, Julai 4, 2021
|
|
Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga, Mhashamu Beatus Urasa, akiwa ameweka mikono juu ya kichwa cha Askofu Mteule wa Jimbo Katoliki Bunda, Simon Chibuga Masondole ikiwa ishara ya kuwekwa wakfu kua Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda, katika viwanja vya Kanisa Kuu Bunda, Mkoani Mara, Julai 4, 2021 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inathamini mchango wa Sekta Binafsi na Taasisi za Dini likiwemo kanisa Katoliki katika kuimarisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii nchini.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Julai 4, 2021) alipomuwakilisha Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya kuwekwa wakafu na kusimikwa kwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bunda, Askofu Simon Chibuga Masondole. Ibada hiyo imefanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu Bunda, Mkoani Mara.
Amesema kuwa Serikali kwa upande wake itaendelea kushirikiana na madhehebu ya dini katika kutoa huduma hizo kwa Watanzania wote bila ubaguzi wa aina yoyote.
“Upo usemi usemao “Kama unataka kwenda haraka tembea peke yako, lakini kama unataka kwenda mbali tembea na wenzako”. Sisi wote tuna imani kubwa nawe kuwa utaendeleza mashirikiano mazuri yaliyopo baina ya Serikali na Kanisa”
Aidha, Waziri Mkuu amewataka Watanzania kutumia nyumba za ibada kuliombea Taifa ili waendelee kuishi kwa amani, upendo na mshikamano.
“Amani tuliyo nayo, ndiyo chachu kubwa ya kufikia mafanikio ya maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi”
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi amesema wataendelea kutoa ushirikiano usio na mashaka kwa askofu mteule na Kanisa Katoliki kwa kuwa wanatambua mchango wa Kanisa hilo katika mkoa wa Mara.