Home BUSINESS NAIBU KATIBU MKUU NISHATI, VIWANDA WATEMBELEA BANDA LA PURA MAONESHO YA SABA...

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI, VIWANDA WATEMBELEA BANDA LA PURA MAONESHO YA SABA SABA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri A. Mahimbali akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA) leo katika maonesho ya 45 ya Saba Saba.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA) leo katika maonesho ya 45 ya Saba Saba. Pembeni yake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri A. Mahimbali.  

DAR ES SALAAM.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri A. Mahimbali na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah watembelea Banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA) kwa lengo la kujionea kazi mbalimbali zinazotekelezwa na Taasisi hiyo katika maonesho ya 45 ya Saba Saba. Viongozi hao walitembelea Banda la PURA siku ya Jumapili tarehe 04 Julai, 2021.

Katika maonesho hayo ya Saba Saba, PURA inaeleza wananchi majukumu mbalimbali inayoyatekeleza yakiwemo kuishauri Serikali juu ya masuala ya mkondo wa juu wa petroli; kusimamia na kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli; na kusimamia shughuli zote za miradi ya kusindika gesi asilia kuwa kimiminika.

Previous articleMAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA TMDA YASHIRIKI MAONESHO YA SABASABA
Next articleWAZIRI MKUU ASHIRIKI IBADA YA MISA TAKATIFU YA KUSIMIKWA ASKOFU SIMONI CHIBUGA MASONDOLE, BUNDA MUSOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here