Home LOCAL WATANZANIA WATAKIWA KUTEMBELEA 77 KUONA MRADI WA JNHPP

WATANZANIA WATAKIWA KUTEMBELEA 77 KUONA MRADI WA JNHPP

DAR ES SALAAM
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili  Stephen Byabato amewataka watanzania kutembelea Banda la Wizara ya Nishati na taasisi zake ili kufahamu na kuona  miradi ya Umeme inayotekelezwa ukiwepo wa Julius Nyerere ( JNHPP)  utakaozalisha megawati 2,115.
Wakili Byayabato alisema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea     banda la Wizara ya Nishati pamoja Taasisi zilizo chini yake katika  Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya  Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Amewaeleza watanzania kutumia maonesho hayo kwenda  kufahamu na kushuhudia  mfano wa bwawa la kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji,( JNHPP).

Amesema kwa kuwa mradi huo unatekelezwa katika eneo ambalo ni vigumu kwa kila mmoja kufika, ni vyema sasa Watanzania wakafika katika banda la Wizara ya Nishati kuona mradi huo mkubwa ambao unatekelezwa  na Serikali yao.

Katika maonesho hayo, Wakili Byabato ametembelea Banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli( PURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja( PBPA).

Tazama picha za matukio mbalimbali kuhusu ziara hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here