Home BUSINESS BALOZI WA UTURUKI AIPONGEZA STAMICO KUANZISHA MRADI WA MKAA MBADALA WA MAKAA...

BALOZI WA UTURUKI AIPONGEZA STAMICO KUANZISHA MRADI WA MKAA MBADALA WA MAKAA YA MAWE

BALOZI wa uturuki nchini Tanzania  Dkt. mehment Guluioliu akiweka saini kitabu maalum cha wageni katika Banda la STAMICO lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Madini Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM.
BALOZI wa uturuki nchini Tanzania  Dkt. mehment Guluioliu. Amelipongeza shirikal la Taifa la Madini  STAMICO kwa kazi kubwa wanayoifanya kwenye sekta ya madini na kadili siku zinavyokwenda wanazidi kuwa wabunifu katika kuhakikisha wananchi wanafaidika la rasilimali hiyo.

Balozi Mehment ambaye amekuwa sehemu ya wageni ambao waliotembelea maonesho ya kimataifa 45 ya sabasaba ambayo yanafanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya kilwa wilayani Temeke.

Amesema kuwa shirika la madini STAMICO wanafanya kazi nzuri sana huku akivutiwa na mradi wa nishati ya mkaa wa mawe ambao wameaza kutekeleza nakwamba mradi huo utaondoa uharibu wa mazingira.

“Mradi wa makaa ya mawe ni mradi mzuri na ni sahihi kwani pamoja na kuwa utafaa kwa matumizi ya majumbani lakini pia utaondo uhalibifu wa ukataji miti hivyo na badala yake watu watatumia nishati ya makaa ya mawe.” Amesema 

Nakuongeza kuwa ” Amefika kwenye Banda la STAMICO .na kupongeza namna hata banda lao linavyovutia na kwamba hata katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu ambacho kimejengwa mkoani mwanza nikazi nzuri sana ya shirika hili “amesema Balozi Mehment .

Amesema kuwa wao kama Uturuki wanaunga mkono juhudi kubwa ambazo zinaendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita chini rais Samia Hassan Suluhu Kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi watanzania Kwa ujumla.

Licha ya Balozi huyo wa uturuki lakini pia viongozi mbalimbali na Balozi wanaowakilishi nchi zao hapa nchini walipata fursa ya kutembelea maonyesho haya ya Sabasaba na kujionea namna wajasiliamali na Wafanyabiashara wamejitokeza.

Mwisho
Previous articlePURA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI NA WADAU MAONESHO YA SABASABA.
Next articleWATANZANIA WATAKIWA KUTEMBELEA 77 KUONA MRADI WA JNHPP

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here