Home LOCAL TCRA KANDA YA ZIWA YAKABIDHI LESENI KITUO KIPYA CHA REDIO CHA GOLD...

TCRA KANDA YA ZIWA YAKABIDHI LESENI KITUO KIPYA CHA REDIO CHA GOLD FM KAHAMA.

Mkurugenzi wa TCRA Kanda ya ziwa Eng.Francis Mihayo Akimkabidhi Leseni Mkurugenzi wa Gold FM Neema Mgeni.
Muonekano wa jengo la kituo kipya cha redio cha Gold fm.

Na: Saimon Mghendi, Kahama.
IMEELEZWA kuwa kuanzishwa kwa kituo kipya cha Gold Fm kwenye Manispaa ya Kahama, Mkoani Shinyanga, kutaleta Mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya Habari katia kanda ya ziwa.

Mkurugenzi wa kituo hicho Neema Mgeni, ameyasema hayo wakati akikabidhiwa leseni hiyo na TCRA Kwenye Mkutano na waandishi wa Habari, Mkutano ambao umefanyika katika Hotel ya Submarine iliyopo katika Manispaa ya Kahama.

Akimkabidhi Leseni hiyo Mkurugenzi wa Gold Fm Mkuu wa TCRA kanda ya Ziwa Eng. Francis Mihayo amekitaka Kituo hicho kuzingatia masharti ya leseni ikiwemo kutumia lugha ambayo imebainishwa kwenye leseni hiyo.
Previous articleTANZANIA YATWAA UBINGWA CECAFA U23
Next articleSHANTA GOLD YAPONGEZWA KUSIMAMIA LOCAL CONTENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here