Home SPORTS SIMBA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA YANGA, YAPIGWA 1-0 DIMBA LA MKAPA DAR.

SIMBA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA YANGA, YAPIGWA 1-0 DIMBA LA MKAPA DAR.

DAR ES SALAAM.

Simba imeshindwa kutangazwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kukubali kichapo cha bao 1_0 dhidi ya Yanga Mechi iliyoshuhudiwa na Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam. 

Shujaa wa Yanga leo ni Kiungo Mkabaji Zawadi Mauya dakika ya 12 kwa shuti kali lililomshinda Mlinda Mlango wa Simba Aishi Manula.

Hii ni mara ya pili kwa Yanga kupata ushindi mbele ya Rais wa Tanzania kwani Msimu uliopita Yanga walishinda Bao moja mbele ya Hayati DK.John Magufuli bao ambalo lilifungwa na Bernard Morrison ambaye yeye leo alikuwa Simba na leo mbele ya Rais Samia imekufa bao moja bila.

Ushindi wa Yanga unaifanya Simba kushindwa kutawazwa bingwa kwa sasa itabidi isubiri mechi nyingine ambapo itashuka Julai 7 uwanja wa Mkapa kucheza na KMC.

Licha ya Yanga kupata ushindi inabaki nafasi ya pili kwa kufikisha Pointi 70 huku Simba ikibaki na pointi 73 na Mechi nne mkononi na Yanga wamebakiza mbili.

Kwa sasa macho na masikio ya watani wa Jadi na mashabiki wao ni Julai 25,2021 uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma watakapocheza Fainali ya Kombe la Azam Sport Federation maarufu kama FA cup.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here