Home LOCAL SERIKALI YATOA MAFUNZO YA UKUSANYAJI MAPATO KWA HALMASHAURI NNE JIJINI ARUSHA.

SERIKALI YATOA MAFUNZO YA UKUSANYAJI MAPATO KWA HALMASHAURI NNE JIJINI ARUSHA.

Katibu Tawala mkoa wa Arusha Athuman Kihamia akiongea na wanahabari baada ya kufungua mafunzo ya uboreshaji wa ukusaji mapato kwa halmashauri nne za mkoa wa Arusha

 

Afisa mwandamizi wa usimamizi wa fedha kutoka TAMISEMI idara ya serikali za mitaa sehemu ya usimamizi wa fedha za mamlaka ya serikali za mitaa Ismail Chami akiongea na wanahabari katika mafunzo ya uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato mkoa Arusha

Mtaalamu mshauri wa mapato ya ndani kutoka GIZ mradi wa GFD Raymond Nzali akielezea  namna wanavyotekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Serikali


Na: Namnyak Kivuyo, Arusha.

Serikali kupitia programu ya utawala bora wa fedha(GFG) inayofadhiliwa na na umoja wa Ulaya, Serikali za Ujerumani na Uswisi na kutekelezwa na shirika la ushirikiano wa kimataifa (GIZ) imetoa mafunzo ya ukusanyaji mapato kwa halmashauri nne za mkoa wa Arusha ambazo ni kati ya halmashauri 21 nchini zilizopo katika programu hiyo.

Akifungua mafunzo hayo katibu tawala mkoa wa Arusha Athumani  Kihamia alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo zaidi wataalamu lakini pia kubadilishana uzoefu na changamoto na fursa na kuweza kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kukusanya mapato zaidi.

“Umuhimu wa kikao hiki ni kuhakikisha kwamba halmashauri zetu 21 Tanzania nne zikiwa za  mkoa wa Arusha zinajengewa uzoefu zaidi,  kama mnavyofahamu mkikusanya mapato mengi ndio mnakuwa na uwezo mkubwa wa kuwatumikia katika kutoa huduma na kuendelea miradi ya maendeleo ambayo lengo lake ni kwenda kupunguza umasikini,”Alisema Kihamia.

Kwa upande wake Ismail Chami Afisa mwandamizi usimamizi wa fedha kutoka TAMISEMI idara ya serikali za  mitaa sehemu ya usimamizi wa fedha za mamlaka ya serikali za mitaa  amesema kuwa wanazo halmashauri 184 nchini ambapo zikiongeza nguvu ukusanyaji wa mapato ambapo zikifanya hivyo zinapunguza utegemezi wa ruzuku kutoka serikali kuu.

Alisema kuwa zimapokusanya mapato mengi zinaboresha huduma kwa wananchi Kama ujenzi wa miundombinu ya barabara, uboreshaji huduma za afya, madarasa na mengineyo lakini bila kuwa na mapato changamoto.

Naye Raymond Nzali mtaalamu  mshauri wa mapato ya ndani kutoka GIZ mradi wa GFG ambapo alisema kuwa wanashirikiana na serikali ya Tanzania kwa kuangazia maeneo makubwa manne  ambayo ni kuimarisha ukaguzi wa fedha kwa kushirikiana na ofisi CAG, kuangalia ukaguzi wa ndani, kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na ushirikishwaji wa jamii.

“Kazi kubwa ya halmashauri na serikali kwa ujumla ni kutoa huduma kwa wananchi na huwezi kutoa huduma kama hauna rasilimali, kwahiyo rasilimali fedha ni nyenzo ya kuweza kusaidia kutoa huduma kwa jamii na ndio maana tumeona kuna haha ya kuweza kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuweza kutoa huduma bora,” Alisema Nzali.

Alifafanua kuwa mradi huo kwa awamu ya kwanza ulianza  mwaka 2016 na kuisha 2020 kwa halmashauri 15 na Sasa wameanza awamu nyingine iliyoanza mwaka 2020 Hadi 2023 kwa kushirikiana na halmashauri 21.

Alieleza kuwa katika eneo la ushirikishwaji wa wananchi wanaotaka waone kwamba wananchi wanaridhika vipi na serikali yao inavyokusanya mapato na jinsi inavyotoa huduma kwasababu wao ndio wanaolipa kodi wanaotaka kupandisha utoaji wa huduma na ukusanyaji wa Kodi ambapo wana mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ndiyo yatashiriki katika hilo ambapo kwa Arusha wa shirika la Angonet na shika la LCDO ambao ndio watakaosaidia kuwaleta wananchi karibu zaidi na serikali yao.

“Tunataka na wenyewe waone umuhimu wa kuchangia mapatoya serikali kwasababu wanapata huduma kwahiyo kwa hizi siku tatu tutakazo kuwepo hapa Arusha lengo letu kubwa ni kuandaa mipango kazi na kuona namna ya kutekelezwa mipango hiyo kulingana na halmashauri husika,” Alieleza.

Hata hivyo halmashauri za mkoa wa Arusha zinazoshiriki katika programu hiyo ni Arusha jiji, Longido, Ngorongoro pamoja na halmashauri ya wilaya ya  Karatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here