Home BUSINESS BOT YAIKUMBUKA SEKTA BINAFSI YAPUNGUZA VIWANGO VYA RIBA KUPAMBANA NA ATHARI ZA...

BOT YAIKUMBUKA SEKTA BINAFSI YAPUNGUZA VIWANGO VYA RIBA KUPAMBANA NA ATHARI ZA UVIKO 19

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga, akisisitiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya BoT leo jijini Dodoma, ambapo BoT imetangaza hatua za kisera zitakazoongeza upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza viwango vya riba ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wetu.

Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina akizungumza kwenye mkutano wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya BoT leo jijini Dodoma.

Waandishi wa habari kwenye mkutano wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga uliofanyika makao makuu ya BoT leo jijini Dodoma.

 DODOMA.

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) katika kupambana na athari za UVIKO-19 imepunguza kiwango cha sehemu ya amana za mabenki kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu ili kuongeza unafuu kwa beki za kibiashara ambapo benki zitakazonufaika zaidi ni zile zitakazotoa mikopo sekta ya kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10.


Hayo yamesemwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Julai 28,2021 ambapo amesema kuwa hatua hizo zilzoanza kufanya kazi Julai 27,2021 zina lengo la kutoa  msukumo mkubwa na kuongeza kasi ya mikopo kwa sekta binafsi  na kupunguza riba ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.


Profesa Luoga amesema kuwa  hatua nyingine waliyoichukua ni kulegeza masharti ya usajili wa mawakala wa benki ambapo waombaji wa uwakala watatakiwa kuwa na kitambulisho cha taifa au namba ya kitambulisho hicho huku hatua nyingine ikiwa ni ukomo wa riba kwenye akaunti za makampuni ya watoa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi ambapo riba itayotolewa katika akaunti hizo haizidi riba itolewayo na benki husika katika amana za akiba.


Aidha Profesa Luoga ameeleza kuwa hatua nyingine ni kuanzishwa kwa mfuko maalum wa kukopesha mabenki na Taasisi za fedha ili ziweze kukopesha Sekta Binafsi ambapo mfuko huo kwa sasa una thamani ya shilingi Trillion 1 na zitatumika kukopesha mabenki na Taasisi za fedha kwa riba ya asilimia 3.


“Hatua hizi za kisera zimechukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya benki kuu ya Tanzania sura ya 197 na Sheria ya mifumo ya malipo ya Taifa sura ya 437 na tutatoa muongozo wa utekelezaji wake kwa mabenki, Taasisi za fedha na makampuni yanoyotoa huduma za kifedha kwa njia ya simu,”Alisema Profesa Luoga.


Amefafanua kuwa janga la UVIKO-19 limeadhiri shughuli za kiuchumi kutokana na nchi zinazofanya biashara kuchukua hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo ikiwemo vizuizi vya safari ambapo kasi ya ukuaji ilipungua kutoka asilimia 7 hadi kufikia asilimia 4.8 kwa mwaka 2020 huku ukuaji wa mikopo ya Sekta Binafsi ukipungua na kati ya asilimia 2.3 hadi  9.1 ambapo pia riba kwa mikopo inayotolewa na Benki za biashara vikiendelea kwa wastani wa asilimia 17.


Pia Ameeleza kuwa uchumi ulikuwa kwa wastani wa asilimia 6.7 kwa kipindi cha 2010-2019 na mfumuko wa bei ulikuwa ikipungua hadi kufikia wastani wa asilimia 3.8 mwaka 2019. 

Previous articleSERIKALI YATOA MAFUNZO YA UKUSANYAJI MAPATO KWA HALMASHAURI NNE JIJINI ARUSHA.
Next articleHABARI KUU ZILIZOPO MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 29-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here