Home BUSINESS MTAALAM WA TIBA MAMA BANGOI AWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA KUONA BIDHAA ZAKE MAONESHO...

MTAALAM WA TIBA MAMA BANGOI AWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA KUONA BIDHAA ZAKE MAONESHO YA SABASABA

DAR ES SALAAM.

MTAALAM mtafiti wa Tiba Aziza Mbeleka Mama Bangoi amewataka Wananchi kutembelea kwenye maonyesho ya kimataifa 45 sabasaba ili kupata huduma ya tiba kutokana na magonjwa mbalimbali yanayowasumbua.

Amesema kuwa yupo kwenye viwanja hivyo vya sabasaba Wilayani Temeke na amekuja dawa za aina mbalimbali ambazo zitaweza kumsaidia mwananchi kutokana na maradhi ambayo anahangaika nayo.

Mama Bangoi amayasema hayo leo ndani ya Viwanja hivyo vya maonyesho wakati Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mtazamano wake katika maonyesho ya 45 Kwa mwaka huu.

Amesema kuwa maonyesho ni mazuri japo bado hayajaaza kuchanganya lakini mwelekeo ni mzuri tu na yeye anapatikana kwenye viwanja hivyo akiwa na aina mbalimbali za tiba na hususani aina za magonjwa yanayowasumbua Binadamu.

Amesema anadawa mbalimbali zinazotimu magonjwa kama vile magonjwa ya akina Mama ,magonjwa ya akina baba,lakini pia kuna dawa inaitwa kumaliza ambayo inatibu magonjwa zaidi ya 200 na imepimwa na mkemia Mkuu wa Serikali.

Pia ameongoza kuwa magonjwa mengine ambayo anatibu ni magoti ,maumivu ya mwili ,mifupa,na visigino kuuma na kuwaka moto ,maumivu ndani ya mwili,maumivu ya misuli,miguu kuvimba ,na maumivu makali ,maumivu ya viungo,kutenguka,katika viungo .

Amesema kuwa katika magonjwa ya akina baba kuziba mkojo, ngiri Maji,fangasi mshipa,ngiri ya tumbo, uume kuvimba,na kuwasha Kwa ndani ,fangasi katika ya mapaja,kujikuna sehemu za siri,haja kubwa .kuongeza nguvu za afya,kinga ya  magonjwa ,kufunga kuharisha, kuoza mwili,pamoja na magonjwa mengine mbalimbali.

Mama Bangoi ambaye baada ya kumalizika Kwa maonyesho ya Sabasaba ofisi zake zipo Tandika Temeke Dar Es Salaam na Kwa mawasiliano yake ili kuweza kupata Tiba yake ni 0754999724.

Amesema mbali nakutoa Tiba lakini pia Bangoi Hebalist clinic imejikita kutoa ushauri mbalimbali juu ya magonjwa hivyo Wananchi watumie fursa hii ya maonyesho ya sabasaba ili kwenda kupata huduma na Tiba Kwa magonjwa mbalimbali ikiwamo kisukari, na magonjwa mengine mengi.

Mwisho..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here