Home BUSINESS TANTRADE YAWAKUTANISHA WADAU WA SEKTA YA NGOZI KUPITIA MIKUTANO YA ANA KWA...

TANTRADE YAWAKUTANISHA WADAU WA SEKTA YA NGOZI KUPITIA MIKUTANO YA ANA KWA ANA MAONESHO YA SABASABA.

AFISA Biashara Mwandamizi wa Tantrade Norah Mishiri (kulia) Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mahojiano maalum mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa ana kwa ana uliowakutanisha wadau wa Sekta ya ngozi kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
AFISA Biashara Mwandamizi wa Tantrade Norah Mishiri akiendeesha mkutano huo ambao pia umefanyika kwa njia ya mtandao ili kutoa fursa kwa wadau wengine walioko nje ya Dar es Salaam na nje ya nchi kushiriki mkutano huo ulioandaliwa na Tantrade kwenye maonesho ya Sabasaba.

Afisa Biashara Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Nyango Mbogola (katikati) akizungumza jambo na Mchumi Mkuu wa Wizara hiyo Chresencia Mwimbwa (kulia) pamoja na Afisa Biashara wa Wizara hiyo Kokuhaisa Katwire (kushoto) mara baada ya kumaliza kwa mkutano wa Ana kwa Ana uliohusu Sekta ya Ngozi kwenye Maonesho ya Sabasaba Dar es Salaam.

Afisa Biashara Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Nyango Mbogola (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa wizara hiyo pamoja na Ofisa wa Tan Trade kwenye Banda la Wizara hiyo kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

AFISA Biashara Mwandamizi  Tantrade Norah Mishiri  amewaomba wadau wajasiriamali kupitia maonesho ya kimataifa ya 45 ya sabasaba kuhudhuria kwenye mikutano ya ana Kwa ana B2B ili kupata maarifa ya kuendesha biashara zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Norah amesema pamoja na mambo mengine wadau kwenye sekta ya ngozi wanajitahidi kutengeneza bidhaa hizo lakini changamoto kubwa ni kwa watumiaji na kwamba ifike mahala wananchi hususani watanzania kuunga jitihada zinazofanywa na wadau kwa kununua bidhaa zao ili kuwafanya waendelee kuzalisha bidhaa hizo kama vile Viatu vya Shuleni ,mabegi na vitu vinginevyo.
“Hapa nataka kusema kuna haja ya kuwaunga mkono wajasiriamali wetu hususani wadau wa bidhaa za ngozi kwani wanatengeneza bidhaa nzuri sana lakini tatizo ni kwenye masoko hivyo tuwaunge mkono.” Amesema.
Ameongeza kuwa hivi sasa inasemekana moja ya changamoto ni wimbi la bidhaa za ngozi kutoka nje ya nchi zinakwamisha soko la ndani Kwa watu wetu lakini wao kama Serikali hawawezi kuzuia uingizaji wa bidhaa hizo kwasababu bado hawajajua uzakishaji wa uhakika wa ndani.
Amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwepo Kwa sera ambayo itarahisha kulitazama eneo la sekta ya bidhaa  za ngozi hapa nchini nakufanya wadau kuwa katika hali nzuri ya kuwepo Kwa soko la uhakika hususani mashuleni.
Mikutano hiyo ya ana Kwa ana inaandaliwa na kuratibiwa na mamlaka ya biashara hapa nchini Tantrade Kwa lengo la kuwajengea uwezo wa wajasiriamali na wadau wengine wa biashara hapa nchini lakini pia ikiwamo kuunganisha Balozi za Tanzania katika kuangizia fursa za kibiashara kwenye nchi husika.
Mwisho.

Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.PILI JULAI 4-2021
Next articleMTAALAM WA TIBA MAMA BANGOI AWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA KUONA BIDHAA ZAKE MAONESHO YA SABASABA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here