Home SPORTS MBUNGE BONAH KUSHIRIKIANA NA MADIWANI KUIBUA VIPAJI SEGEREA

MBUNGE BONAH KUSHIRIKIANA NA MADIWANI KUIBUA VIPAJI SEGEREA

Mbunge wa Jimbo LA Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akikagua timu ya Mpira miguu Kata ya Kipawa Wilayani Ilala katika mashindano yalioandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Aidan Kwezi Jana Julai 17/2021 Katikati NAIBU Meya Halmashauri ya Jiji Saady KIMJI (PICHA na HERI SHAABAN)

Mbunge wa Jimbo LA Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akisalimiana na Diwani wa Kata ya Buguruni Mnyamani Shukuru Dege katika mashindano yalioandaliwa na Diwani wa Kata ya Kipawa Aidani Kwezi (Katikati) Jana Julai 17/2021 (PICHA. Na HERI SHAABAN)

NAIBU Meya wa Halmashauri ya Jiji Saady KIMJI akisalimiana na Diwani wa Kata ya Kipawa Aidani Kwezi Katika mashindano ya ufunguzi wa Kombe LA kugombea ngombe viwanja vya Shule ya Msingi Majani ya Chai Julai 17/2021 (PICHA NA HERI SHAABAN)
NAIBU Meya wa Halmashauri ya Jiji Saady KIMJI akikagua timu ya wanawake katika mashindano yalioandaliwa na Diwani wa Kata Kipawa Aidani Kwezi Jana Julai, 17/2021 (PICHA NA  HERI SHAABAN)

NA: HERI SHAABAN (ILALA)

MBUNGE  wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli, amesema ataendelea kushirikiana na madiwani wote wa jimbo hilo kuibua vipaji vya vijana katika michezo mbalimbali.

Bonnah ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Kipawa (Kipawa Diwani Cup), amesema licha ya michezo kujenga afya pia ni ajira.

“Nampongeza diwani kwa kuandaa mashindano haya yanasaidia kuwaweka vijana karibu, mpira ni afya lakini mpira ni ajira kwa sababu vijana wengi wanaanzia chini, wanaanza katika timu ndogondogo hadi wanafikia hatua ya kucheza timu kubwa. Kwahiyo nitaendelea kushirikiana na madiwani ili tuibue vipaji vingi vya vijana na pia tutaandaa mashindano ngazi ya jimbo,” amesema Bonnah.

Naye Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saad Khimji, amewataka madiwani wengine waige mfano wa Kwezi kwa kuandaa mashindano kama hayo ili kuacha kumbukumbu katika maeneo wanayoongoza.

“Ni vema madiwani tukawa na jambo ambalo tutakuwa tunalifanya kila mwaka kwa ajili ya kuacha kumbukumbu katika maeneo tunayaongoza, suala la mpira si burudani tu au afya, michezo kwa ujumla ni ajira kwa vijana. Vijana wengi sana wamenufaika kupitia mpira wa miguu mfano Mbwana Samata ameanzia kwenye michezo kama hii,” amesema Khimji.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kipawa, Aidan Kwezi, amesema kata hiyo ina vipaji vingi lakini katika miaka ya karibuni michezo ilikuwa imelala kwahiyo amejipanga kuiinua.

“Nilivyoingia kwenye nafasi hii mwaka 2020 moja ya malengo yangu ni kuhakikisha tunainua michezo na kuwakusanya vijana pamoja ili tuweze pia kushirikishana mambo mengine ya kuinuana kiuchumi,” amesema Kwezi.

Amesema mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atapata ng’ombe mwenye thamani ya Sh milioni moja wakati mshindi wa pili atapata mbuzi na mpira na timu nane zitakazoingia kwenye hatua ya robo fainali zitapata jezi. Pia kutakuwa na zawadi za mfungaji bora, kipa bora na kikundi bora cha ushangiliaji.

Katika ufunguzi wa mashindano hayo uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Majani ya Chai, timu ya FC Bontown iliibuka mshindi kwa kupata mabao 2 – 1 dhidi Falsafa FC.

Mashindano hayo yatahusisha timu 32 za mpira wa miguu na timu nane za mpira wa pete.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here