Home LOCAL MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI SOKO LA KISASA...

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI SOKO LA KISASA JIDA MJINI MASASI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasili kat ya Jida kuweka jiwe la msingi Soko la wafanyabiashara ndogondogo la Jida lililopo Wilaya ya Masasi. Soko hilo linagharimu shilingi milioni 619.9.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka kwa Leonard Mkondola ambaye ni Fundi Mchundo wa soko la kisasa la Jida mara baada ya kuwasili kuweka jiwe la msingi sokoni hapo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiweka jiwe la msingi soko la kisasa la Jida lililopo Wilaya ya Masasi ambalo limejengwa kwaajili ya wafanyabiashara wadogo.

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza wakati alipofika kuweka jiwe la msingi katika soko la kisasa la Jida lililopo Wilaya ya Masasi.
Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya mara baada ya kukagua majengo ya stendi ya mabasi ya Mangaka. Makamu wa Rais aliagiza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi huyo ili kupisha uchunguzi kufuatia matumizi mabaya ya fedha za mradi huo.

Previous articleTANZANIA YAPOKEA ZAIDI YA DOZI MILIONI 1 YA CHANJO YA COVID-19 KUTOKA MAREKANI
Next articleTANZANIA RECEIVES COVID-19 VACCINES FROM THE US

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here