Na,Saimon Mghendi, KAHAMA
Afisa madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini Kahama Eng. Joseph Kumburu amewaonya baadhi ya wachimbaji wadogo Wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Kabela wanaoshirikiana na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kutorosha madini.
Kumburu ameyasema hayo jana katika mkutano maalumu na wachimbaji hao, mkutano ambao umefanyika katika ofisi za mgodi wa Kabela uliopo katika kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama, na kudhuriwa na makundi ya wadau wa madini.
“Hapa tumefanya operationi siku moja tu sokoni kumepatikana gramu 1000 kutoka gramu 300, pale sokoni dhahabu haiendi na hao makota mnao wasema ndio wanatuibia na walio kamatwa wote ni makota na wanasema nikweli hupeleka dhahabu nusu sokoni na wao huchukua nusu”,alifafanua Eng. Kumburu.
Kwa upande wake katibu wa mgodi wa Kabela Jomanga Mzee amesema kuwa wataakikisha wanakomesha Hali hiyo pamoja na kitekeleza maelekezo yote waliopewa na Serekali.
Hata hivyo wachimbaji wadogo wakitoa changamoto zao mbele ya afisa madini mkazi wa Mkoa wa Kimadini Kahama, Emanuel Kazoba na Rosemary Mamba, wameiomba serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri yatakayo wawezesha kuuza dhahabu hata kwa wanunuzi wadogowadogo maarufu kama Makota.
Akitolea Ufafanuzi wa Sheria ya Madini kwa Wachimbaji hao Eng. Kumburu, Alisema kuwa Kota Atambuliki Kisheria