Home BUSINESS PROF.MKUMBO AZINDUA TELA MAALUMU KWAAJILI YA MKULIMA KATIKA BANDA LA NDC SABASABA

PROF.MKUMBO AZINDUA TELA MAALUMU KWAAJILI YA MKULIMA KATIKA BANDA LA NDC SABASABA

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akizindua tela maalumu kwaajili ya kubebea mazao kwa mkulima. Uzinduzi umefanyika katika banda la NDC katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yabayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari katika Uzinduzi wa tela maalumu kwaajili ya kubebea mazao kwa mkulima. Uzinduzi umefanyika katika banda la NDC katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yabayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo (wa pili kulia) akipata picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (wa kwanza kulia), MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutageruka (wa kwanza kushoto),  na Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Bi.Rhobi Sattima mara baada ya kuzindua tela maalumu kwaajili ya kubebea mazao ya mkulima.Uzinduzi umefanyika katika banda la NDC katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yabayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.


NA: EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo ameipongeza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa kushirikiana na TEMDO pamoja na CARMATEC kuhakikisha kiwanda inachokisimamia cha KMTC kinatengeneza tela ambalo litasaidia kubeba mazao na bidhaa kwa wakulima.

Akizungumza uzinduzi  wa tela hilo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere  JijiniDar es Salaam, Prof.Mkumbo amesema tela hilo linauzwa kwa bei ya shilingi milioni 8.3 ambalo unaweza kulliweka vijijini na kuweza kuajiri vijana wengi waliopo mtaani na kuwaingizia kipato katika kipindi cha mavuno.

“Tela hili limetengenezwa hapa hapa Tanzania , ambapo  kiwanda chetu cha KMTC kipo, hii inaonesha kwamba viwanda vyetu kwakweli vinaweza kutengeneza bidhaa za msingi  na moja ya malengo yetu ni kukidhi mahitaji ya soko la ndani ili tuanze kutumia na kula bidhaa ambazo tunazalisha sisi wenyewe hapa”. Amesema Prof.Mkumbo.

Nae Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe amesema uzinduzi wa tela hilo utaenda kuongeza thamani ya uzalishaji hasa katika sekta ya kilimo ambapo moja wapo ya changamoto kubwa ni kwenye usafirishaji mazao na bidhaa mbalimbali.

” Bidhaa zinakuwa zinaharibika au kutokufika kwa urahisi katika maeneo husika kwasababu ya kukosa vifaa maalumu na vya bei rahisi kwaajili ya kusafirishia mazao hayo na bidhaa mbalimbali”. Amesema Mhe.Kigahe.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la maendeleo  (NDC), Bi.Rhobi Sattima amesema kuwa tela hilo lenye uwezo wa kubeba tani tano limebuniwa kwa kuzingatia vigezo vyote vya ubora, ufanisi na usalama wakati linapokuwa linafanya kazi na kuthibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Amesema kuwa tela hilo limetokana na wazo bunifu la kuwa na chombo cha kusafirisha pembejeo na mazao ya kilimo  ambalo litakokotwa na trekta linalounganishwa katika kiwanda cha matrekta  kilichopo katika eneo la mitaa ya Viwanda  TAMCO, Kibaha.

“Tela hili limesafiniwa kwa ushirikiano kati ya  NDC,TEMDO na CARMATEC. NDC walitoa wazo bunifu, TEMDO walihusika katika usanifu na michoro na CARMATEC walihusika katika  kufanya majaribio ya tela hili”. Amesema Bi.Sattima.

Amesema moja ya mchango wa tela hilo kwenye uchumi ni  pamoja na mapinduzi kwenye sekta ya kilimokwani mkulima  anaweza kuzalisha bila ya kuwa na changamoto ya usafirishaji wa mazao na pembejeo.Hii itasaidia kypatikana kwa urahisi malighafi za kilimo kwa ajili ya uongezaji thamani katika viwanda.

 

Previous articleKUMBURU AWAPA ONYO KALI WACHIMBAJI WANAOTOROSHA DHAHABU
Next article

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here