Home LOCAL NISHATI INAAKISI KAULIMBIU YA MAONESHO YA SABASABA : NAIBU WAZIRI MAHIMBALI.

NISHATI INAAKISI KAULIMBIU YA MAONESHO YA SABASABA : NAIBU WAZIRI MAHIMBALI.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah wakipata maelezo mara baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 4,2021.

Kaimu Meneja Miradi, Mipango na Utafiti kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Jensen Mahavile akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah masuala ya umeme vijijini mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 4,2021.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah wakiangalia mita za umeme zinazozalishwa hapa nchini katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 4,2021.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah wakiangalia majiko yanayotumia teknolojia ya sumaku katika Banda la Wakala wa Nishati Vijijini katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 4,2021.

Mhandisi Mradi kutoka mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah kuhusu mradi huo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 4,2021.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah vitabu vya Sera ya Nishati pamoja Mpango Kabambe wa Umeme mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 4,2021.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, akisaini kitabu cha wageni baada kutembelea Banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli( PURA) katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 4,2021.

 

Na: Teresia Mhagama na Zuena Msuya, DSM

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali amesema sekta ya nishati inaakisi kauli mbiu ya Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ambayo ni Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu.

Mahimbali alisema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea baadhi ya mabanda ya washiriki wa Maonesho hayo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, mkoani Dar es Salaam, Julai 4, 2021, ambapo aliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah

Alifafanua kuwa nishati inaakisi kauli mbiu ya Maonyesho hayo kwa kuwa vitu vyote vilivyolengwa katika kauli mbiu hiyo vinategemea zaidi uwepo wa nishati ya uhakika katika utekelezaji wake.

“Nimefarijika sana kutembelea maonesho haya ya Sabasaba, nimewasikiliza wafanyabiashara kila mmoja kwa nafasi yake amekuwa  akizungumzia nishati ya Umeme kwa namna ambavyo  anaitumia kuboresha Biashara yake kwa namna moja ama nyingine kwa maeneo ya vijijini ni Mijini”, alisema Mahimbali

Aliongeza kuwa, inadhihirisha wazi kuwa nishati ya Umeme ni mkombozi mkubwa wa ukuaji wa uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja.

Aidha aliwaasa watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea Banda la Nishati pamoja na Taasisi zake, ili kuona, kujifunza na kupata uelewa zaidi juu ya shughuli zinazofanywa na wizara pamoja na Taasisi zake.

Vilevile aliwaeleza watanzania kuwa wafike katika mabanda hayo ili kuona mfano wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme wa megawati 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, pamoja na kupata maelezo ya namna mradi huo unavyotekelezwa na hatua iliyofikiwa hadi sasa katika ujenzi wake.

Aliongeza kuwa katika maonesho hayo, watanzania wataona namna ambavyo Joto Ardhi inavyozalisha umeme kwa kutumia mvuke unaotoka chini ya ardhi.

Pia, aliwakumbusha watanzania kutumia nishati ya Umeme katika kujiletea maendeleo kwa kuwa serikali inatumia nguvu kubwa kuhakikisha kuwa nishati hiyo inasambazwa nchi nzima kwa gharama nafuu.

Sambasamba na hilo, watapata maelezo kwa kina kuhusu gharama za kunganishiwa umeme katika nyumba kazoo katika maeneo mbalimbali nchini, na matumizi sahihi ya umeme.

Akiwa katika viwanja hivyo vya Mwalimu Nyerere, Mahimbali alitembelea mabanda mbalimbali ikiwepo la Wizara ya Nishati na taasisi zilizochini yake ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Kampuni ya Uendelezaji Joto Ardhi ( TGDC), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja( PBPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Mamlaka ua Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA).

 

Previous articleUBUNIFU WA WAJASIRIAMALI WA TWCC WAVUTIA WENGI MAONESHO YA SABASABA
Next articleKUMBURU AWAPA ONYO KALI WACHIMBAJI WANAOTOROSHA DHAHABU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here