Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imenyakua makombe mawili kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45, moja likiwa la Mshindi wa Tatu wa Jumla na lingine likiwa la Mshindi wa Kwanza kwa Taasisi.
|
||
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Uendeshaji BoT, Bw. Kened Nyoni Afisa Rasimali Watu Mwandamizi, akijadili jambo na Bi. Consolata Shao, kwenye banda la BoT Sabasaba.
Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Missango, akipewa maelezo kuhusu Dhamana za Serikali na Mchambuzi wa Masuala ya Fedha, Bw. Martin Kalihose, kwenye banda la BoT Sabasaba.
Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina, akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa BoT, Bw. Benard Dadi, katika majadiliano na Mchambuzi wa Mifumo, Bw. Robert Masalu na Mchambuzi wa Fedha Mwandamizi, Bi. Kidee Mshihiri
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani BoT, Bi. Aziza Hamis (kulia) akipewa maelezo kuhusu Maendeleo ya Uchumi wa Tanzania na Mchumi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bi. Sylvia Bwakea.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mifumo ya TEHAMA, Bw. Joel Ngussa, Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha, Bw. Alexander Ng’winamila, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Missango, Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Jamhuri Ngelime, Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, Bw. Augustino Hotay, Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu, Bw. Nixon Kyando na Afisa Benki Mkuu Mwandamizi, Bi. Restituta Minja kwenye banda la BoT Sabasaba.
Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bw. Richard Malisa (kushoto) akijadiliana jambo na Afisa Rasimali Watu Mwandamizi, Bi. Joyce Shala na Afisa Benki, Bi. Rukia Muhaji.