DAR ES SALAAM.
BALOZI wa uturuki nchini Tanzania Dkt. mehment Guluioliu. Amelipongeza shirikal la Taifa la Madini STAMICO kwa kazi kubwa wanayoifanya kwenye sekta ya madini na kadili siku zinavyokwenda wanazidi kuwa wabunifu katika kuhakikisha wananchi wanafaidika la rasilimali hiyo.
Balozi Mehment ambaye amekuwa sehemu ya wageni ambao waliotembelea maonesho ya kimataifa 45 ya sabasaba ambayo yanafanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya kilwa wilayani Temeke.
Amesema kuwa shirika la madini STAMICO wanafanya kazi nzuri sana huku akivutiwa na mradi wa nishati ya mkaa wa mawe ambao wameaza kutekeleza nakwamba mradi huo utaondoa uharibu wa mazingira.
“Mradi wa makaa ya mawe ni mradi mzuri na ni sahihi kwani pamoja na kuwa utafaa kwa matumizi ya majumbani lakini pia utaondo uhalibifu wa ukataji miti hivyo na badala yake watu watatumia nishati ya makaa ya mawe.” Amesema
Nakuongeza kuwa ” Amefika kwenye Banda la STAMICO .na kupongeza namna hata banda lao linavyovutia na kwamba hata katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu ambacho kimejengwa mkoani mwanza nikazi nzuri sana ya shirika hili “amesema Balozi Mehment .
Amesema kuwa wao kama Uturuki wanaunga mkono juhudi kubwa ambazo zinaendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita chini rais Samia Hassan Suluhu Kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi watanzania Kwa ujumla.
Licha ya Balozi huyo wa uturuki lakini pia viongozi mbalimbali na Balozi wanaowakilishi nchi zao hapa nchini walipata fursa ya kutembelea maonyesho haya ya Sabasaba na kujionea namna wajasiliamali na Wafanyabiashara wamejitokeza.
Mwisho