Home LOCAL BILIONEA LAIZER AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIANA NA SERIKALI KUISAIDIA JAMII

BILIONEA LAIZER AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIANA NA SERIKALI KUISAIDIA JAMII

 

DAR ES SALAAM.
BILIONEA mtanzania Saniniu Laizer ameshauri kuwa watanzania wajenga nidhamu ya kusaidia Jamii inayowazunguka  japo kidogo pindi wanapopata mafanikio kwani kufanya hivyo kunaongeza baraka katika shughuli zako.

Leizer ameyasema hayo leo kupitia maonyesho ya kimataifa ya 45 ya sabasaba ambayo yanaendelea wilayani temeke ambapo amesema kuwa anajisikia faraja sana kwamba anakuwa sehemu ya wadau wanaotambua changamoto zilizopo kwenye jamii hususani wilayani kwake Simanjiro.

Amesema katika siku za hivi karibuni katika kidogo ambacho anakipata kupitia shughuli zake za madini amekabidhi Shule ya Msingi  yenye vyumba Saba ,nyumba za walimu mbili pamoja na matundu ya vyoo kumi kwa uongozi wa serikali ya wilaya hiyo.

Ameongeza kuwa kwa kutambua mchango wake huo kwenye sekta ya elimu Shule hiyo  imepewa jina lake la Saniniu na imejengwa katika Kijiji Cha Naepo kilichopo kata ya Naisinyai wilayani humo ambapo imetumia zaidi ya shilingi milioni 466 hadi kukamilika kwake.

Laizer ambaye amekuwa kivutio kwenye maonyesho hayo ya Sabasaba kutoka na ushiriki wake Mwaka huu huku  Banda la Sekta ya Madini likipambwa na Picha za bilionea huyo wa Madini ya Tanzanite nchini.

Laizer amesema maonyesho ni mazuri na kubwa zaidi amekuwa akishirikiana vizuri na serikali na ndio maana yupo bega kwa bega na amekuwa akisaidia pindi anapopata fursa ya kufanya hivyo .

“wakati mwingine kusaidia kunahitaji uzalendo ,upendo thabiti dhidi ya Taifa lako lakini kubwa zaidi kujitoa hivyo nashukuru kwa kufanikisha ujenzi wa shule hiyo ambayo kimsingi niliaza kuijenga mwaka 2017.” Amesema Leizera wakati akihojiana na waandishi wa habari kwenye maonyesho hayo.

Akizungumzia ushirikiano wake na Jamii inayomzunguka leizer amesema wanashirikiana vizuri na hana tatizo na mtu yeyote na kubwa zaidi anachokifanya nikuona anasaidia Jamii kadri anavyojaliwa na Mwenyezi Mungu na si vinginevyo.

Katika hatua nyingine Bilionea Laizer ameipongeza wizara ya madini kwa ushirikiano mkubwa wanaompatia hali ambayo imewezesha kufikia hatua aliyonayo na kwamba ataendelea kushirikiana na serikali katika  kuunga mkono juhudi zake kadri atakavyokuwa anabarikiwa 

Katika kipindi hichi cha maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba amewataka watanzania kujitokeza Kwa wingi ili kupata elimu ya Madini na hasa Madini ya Tanzania ambayo yanapatikana nchini tu.na wafike kwenye Banda la wizara ya Madini watakutana na Banda la leizer watapata elimu hapo.

Mwisho.
Previous articlePURA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI NA WADAU MAONESHO YA SABASABA.
Next articleWATANZANIA WATAKIWA KUTEMBELEA 77 KUONA MRADI WA JNHPP

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here