Home LOCAL BALOZI MULAMULA AAPA KUWA MBUNGE EALA

BALOZI MULAMULA AAPA KUWA MBUNGE EALA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameapa kuwa mjumbe wa maamuzi wa Bunge la Afrika Mashariki (AELA). Balozi Mulamula ameapa kuwa mjumbe wa maamuzi wa EALA leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam. Picha na Mambo ya Nje. 

DAR ES SALAAM.

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge hilo leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam

Akizungumza mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam Balozi Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na umuhimu  na matarajio ya Wananchi kwa Bunge hilo.

Aidha Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

“Wananchi wamekuwa na matarajio makubwa sana kupitia Bunge hili la Afrika Mashariki kiuweza kuona faida na mambo mazuri yanayofanyika kupitia jumuiya hii ya Afrika Mashariki,” Amesema Balozi Mulamula.

Previous articleUJENZI MJI WA SERIKALI MTUMBA
Next articleWANANCHI MBALIMBALI WAENDELEA KUPATA ELIMU YA HUDUMA ZA KIFEDHA KWENYE BANDA LA BoT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here