Home SPORTS YACOUBA SONGNE AIPELEKA YANGA SC FAINAL KOMBE LA AZAM SPORTS ...

YACOUBA SONGNE AIPELEKA YANGA SC FAINAL KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION (FA).

TABORA.

Tiimu ya Yanga SC imefanikiwa kufuvu kuingia hatua ya Fainali ya Kombe la Azam Sports Federation maarufu kama  (FA) baada ya kuitandika timu ya Biashara United ya mjini Musoma mchezo uliochezwa katika Dimba la Ally Hassan Mwinyi Mjini Tabora.

Kiungo Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne aliitanguliza Yanga kuongoza kwa bao moja alipopachika bao hilo katika dakika ya 22 ya kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa kiungo wa kati Feisal Salum (Fei Toto) na kuifanya Yanga kumaliza mchezo huo kwa kushinda 1-0.

Kufuatia ushindi huo sasa wana Jangwani hao wanasubiri kucheza fainali ya Michuano hiyo na timu kati ya Simba ya SC na Azam FC mchezo utakaopigwa kesho katika Dimbani la Majimaji Mjini Songea 


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here