Home LOCAL SIMBACHAWENE ARIDHISHWA NA KASI UJENZI MAKAZI YA ASKARI ZIMAMOTO, KUKAMILIKA SEPTEMBA MWAKA...

SIMBACHAWENE ARIDHISHWA NA KASI UJENZI MAKAZI YA ASKARI ZIMAMOTO, KUKAMILIKA SEPTEMBA MWAKA HUU.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati), akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF John Masunga (kulia), baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa makazi ya Askari wa Jeshi hilo, unaoendelea kujengwa katika eneo la Kikombo, jijini Dodoma.  Simbachawene ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambapo ukikamilika utasaidia familia 80 ya Askari kuishi katika makazi hayo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimpa maelekezo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF John Masunga, baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa makazi ya Askari wa Jeshi hilo, unaoendelea kujengwa katika eneo la Kikombo, jijini Dodoma.  Simbachawene ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambapo ukikamilika utasaidia familia 80 ya Askari kuishi katika makazi hayo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akimpa maelekezo Mhandisi wa Ujenzi wa Makazi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakati alipokuwa anafanya ukaguzi wa makazi hayo yanayoendelea kujengwa katika eneo la Kikombo, jijini Dodoma, leo.  Simbachawene ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambapo ukikamilika utasaidia familia 80 ya Askari kuishi katika makazi hayo. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, CGF John Masunga.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati), akiangalia ramani ya ujenzi wa makazi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, yaliyopo Kikombo, jijini Dodoma, leo, wakati alipokuwa anafanya ziara ya kukagua ujenzi huo unaoendelea. Simbachawene ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambapo ukikamilika utasaidia familia 80 ya Askari kuishi katika makazi hayo. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, CGF John Masunga, na kushoto ni Mmiliki Majengo wa Jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Julius Ntabala.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akikagua ujenzi wa makazi ya askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, yaliyopo Kikombo, jijini Dodoma. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, CGF John Masunga. Simbachawene ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo hayo ambayo ukikamilika utasaidia familia 80 ya Askari kuishi katika makazi hayo. Kushoto ni Mmiliki Majengo wa Jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Julius Ntabala.

Na: Mwandishi Wetu, MoHA, Dodoma

KATIKA kukabiliana na uhaba wa nyumba za watumishi nchini, Serikali imetoa shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa makazi  ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika eneo la Kikombo Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amezungumza hayo, jijini Dodoma, leo, mara baada ya kukagua ujenzi huo huku akifurahishwa na kuridhishwa namna ambavyo ujenzi unavyoendelea.

Alisema ameridhika na namna ya gharama za ujenzi wa makazi hayo yenye majengo sita na gharama zinavyokwenda na kujidhihirisha kwamba bilioni tano zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zinatumika kiuhalali na fedha hizo zitamaliza ujenzi huo.

“Nimefurahishwa sana na kasi ya ujenzi, nimeridhika na ujenzi unaoendelea ujenzi wa mradi huu wa nyumba za Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, nikupongeze Kamishna Jenerali kwa kusimamia vema fedha za Serikali inaonyesha dhahiri kwamba kazi itakamilika kwa ufanisi,” alisema Simbachawene.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali, John Masunga alisema nyumba hizo zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa mwaka na askari pekee ndio watakaa katika makazi hayo na sio maafisa.

Alisema kukamilika kwa nyumba hizo itakuwa mkombozi mkubwa kumaliza kilio cha wa Askari ambao wanakabiliwa na makazi ya kuishi na kwamba nyumba hizo ni maalumu kwa Askari wa chini na ambao wanafanya kazi ofisi ya Makao Makuu na kituo cha Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chamwino.

“Tunaishukuru sana Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto hii na kutupatia fedha hizo tunamuahidi  tutajitahidi tunamaliza makazi haya kwa wakati,” alisema CGF Masunga.

Akisoma taarifa ya miradi inayotekelezwa na Jeshi hilo, Mmliki Majengo wa Jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Julius Ntabala alisema kuwa Jeshi hilo kwa Mwaka 2020/21 linatekeleza miradi mitatu ikiwemo Kituo cha Zimamoto na Uokoaji eneo la Chamwino, ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji eneo la Nzuguni na mradi wa Makazi ya Askari Kikombo.

Akifafanua namna mradi ulipofikia alisema ujenzi makazi ya Kikombo yako hatua ya asilimia 55 ambayo ipo hatua ya kupaua na kuanza kazi za ndani na nje na kwamba kwa sasa kazi inayoendelea ni ufungaji wa nondo za sakafu ya ghorofa ya nne na kisha kumwaga zege la nguzo na kupandisha kuta na kuweka mkanda wa mwisho.

“Ujenzi unaendelea vizuri gharama zilizotumika mpaka sasa ni shilingi 4,006,486,300.00 mbali na jitihada hizi tumekumbana na changamoto ya kupanga kwa gharama za saruji ambapo kumeathiri mradi na tutakapofika mwishoni tutaona mapungufu ni kiasi gani kimepungua ili tuombe fedha ya nyongeza,” alisema Ntabala.

Previous articleTAASISI ZA SANAA ZITUMIKE KUENDELEZA SANAA
Next articleYACOUBA SONGNE AIPELEKA YANGA SC FAINAL KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION (FA).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here