Na: Saimon Mghendi, KAHAMA
Naibu Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Pauline Gekul Amewapongeza wakurugenzi wa Ukumbi wa burudani wa THE MAGIC 101 uliopa katika Manispaa Ya Kahama kwa kuja na wazo la kuanzisha ukumbi huo jambo ambalo limepelekea vijana Zaidi ya 60 kupata ajira.
Gekul ameyasema hayo leo wakati akizindua Ukumbi wa kisasa wa burudani wa THE MAGIC 101, uliopo katika manispaa ya Kahama, Ukumbi ambao umejengwa na wawekzaji wazawa na kutumia Zaidi ya Tsh. Milioni miatano.
“Kuna watu wamemuelewa Rais wetu Mama Samia, kwamba ajira sio lazima tukae ofisini tukalipwa mishahara mwisho wa mwezi, kumbe sisi tunaweza tukasimama na tukatoa ajira kwa wenzetu, uwekezaji uliofanyika hapa ni mkubwa kwahiyo ndugu zetu lazima tuwapongeze”, amesema Waziri Gekul.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo kiswaga, amesema kuwa moja kati ya vipaumbele vyake nikuona wana Kahama wakifanya kazi kwa bidi ya uzalishaji mali, lakini pia wanapata sehemu nzuri za mapumziko kwa ajili ya kuburudika.
Nae mmoja kati ya wamilki wa Ukumbi huo wa Burudani, Emanuel Kabekeza, wakati akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya mgeni rasimi, amesema kuwa ndoto yao kama vijana ni kujiinua kiuchumi, kulipa kodi kwa serekali lakini kubwa zaidi ni kutengeneza fursa kwa vijana wa Tanzania.