Home ENTERTAINMENTS WAZIRI GEKUL AWAPONGEZA WAKURUGENZI WA MAGIC 101 KWA KUTOA AJIRA KWA VIJANA

WAZIRI GEKUL AWAPONGEZA WAKURUGENZI WA MAGIC 101 KWA KUTOA AJIRA KWA VIJANA


Naibu Waziri Habari wa Habari,Utamaduni,michezo na sana na Mkuu wa  Wilaya ya Kahama Pamoja na Wakurugenzi wa MAGIC 101 kwnye uzinduzi wa Ukumbi wa kisasa wa THE MAGIC 101.

Naibu Waziri Habari wa Habari,Utamaduni,michezo na sanaa  paamoja na Mkuu wa  Wilaya ya Kahama wakikagua maeneo mbalimbaliya Ukumbi huo kabla ya kuufungua rasimi.

Waziri Habari wa Habari,Utamaduni,michezo na sanaa  kwenye picha ya paamoja na Mkuu wa  Wilaya ya Kahama Pamoja na Wakurugenzi wa MAGIC 101.

Muonekano wa Ukumbi huo wa burudani 

Na: Saimon Mghendi, KAHAMA

Naibu Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Pauline Gekul Amewapongeza wakurugenzi wa Ukumbi wa burudani wa THE MAGIC 101 uliopa katika Manispaa Ya Kahama kwa kuja na wazo la kuanzisha ukumbi huo jambo ambalo limepelekea vijana Zaidi ya 60 kupata ajira.

Gekul ameyasema hayo leo wakati akizindua Ukumbi wa kisasa wa burudani wa THE MAGIC 101, uliopo katika manispaa ya Kahama, Ukumbi ambao umejengwa na  wawekzaji wazawa na kutumia Zaidi ya Tsh. Milioni miatano.

“Kuna watu wamemuelewa Rais wetu Mama Samia, kwamba ajira sio lazima tukae ofisini tukalipwa mishahara mwisho wa mwezi, kumbe sisi tunaweza tukasimama na tukatoa ajira kwa wenzetu, uwekezaji uliofanyika hapa ni mkubwa kwahiyo ndugu zetu lazima tuwapongeze”, amesema Waziri Gekul.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo kiswaga,  amesema kuwa moja kati ya vipaumbele vyake nikuona wana Kahama wakifanya kazi kwa bidi ya uzalishaji mali, lakini pia wanapata sehemu nzuri za mapumziko kwa ajili ya  kuburudika.

Nae mmoja kati ya wamilki wa Ukumbi huo wa Burudani, Emanuel Kabekeza, wakati akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya mgeni rasimi, amesema kuwa ndoto yao kama vijana ni kujiinua kiuchumi, kulipa kodi kwa serekali lakini kubwa zaidi ni kutengeneza fursa kwa vijana wa Tanzania.


Previous articleKAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YAAGIZA WMA NA WRRB KUENDELEA KUBORESHA UTENDAJI KAZI NA UTOAJI WA HUDUMA
Next articleRAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 12 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA JIJINI DAR.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here