Home BUSINESS WAFANYABIASHARA NCHINI WATAKIWA KUTUMIA BRELA KUSAJILI BIASHARA ZAO

WAFANYABIASHARA NCHINI WATAKIWA KUTUMIA BRELA KUSAJILI BIASHARA ZAO

 

WAFANYABIASHARA nchini wametakiwa kutumia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kuweza kujisajili ili kuwawezesha kupata ulinzi shughuli zao hivyo pia kuwarahisishia kuweza kupata mikopo benki.

Hayo yalisemwa na Afisa Usajili Msaidizi Idara ya Makampuni majina ya Biashara kutoka Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (Brela) Marry Glory Mmari (Pichani ) wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya biashara yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya Mwahako mjini hapa.

Alisema wafanyabiashara hao wanapokuwa wamesajiliwa kisheria na kupata majina ya biashara zao inawawezesha hata wakati wanapokuwa wakiomba mikopo benki kupata kirahisi kutokana na kwamba benki wanaweza kucheki nao na kuwaeleza huyo mtu amesajiliwa.

“Hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashara ambao hawajasajili watumie brela kusajili biashara zao kwani inakuwa faida kwao kutokana na kwamba anakuwa amepata ulinzi hivyo kumrahisishia kwenda benki kupata mikopo”Alisema Marry Glory.

Hata hivyo alisema wameendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara ,wananchi na wajasiriamali kuhusu shughuli wanazozifanya na mwamko umekuwa mkubwa ambapo zaidi ya majina ya Biashara 30 na makampuni 10 ikiwemo kuhuisha taarifa majina 10 ya biashara kutoka kwenye mfumo wa zamani.

Alisema taarifa hizo zilihuhishwa kutoka kwenye mfumo wa zamani kwenye kieletroniki huku akieleza changamoto kubwa zilizokuwepo wakati wa kubailisha mfumo alikuwa ni kazi kubwa kama mteja anakuwa amesahau taariufa zake.

Hata hivyo alisema ili mteja aweze kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa na akaunti, aina ya jina analosajili na namba ya nida ikiwemo simu na barua pepe ili aweza kusajili jina la biashara.

“Kwa kweli tunashukuru mwitiko umekuwa mkubwa sana lakini pia tumeweza kuwafikia watu mbalimbali ambao walishiriki kwenye maonyesho hayo hivyo tuendelee kuwahimiza watanzania kusajili biashara zao “Alisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here