Home LOCAL TANZANIA NA KOREA KUSINI WATIA SAINI MAENEO YA USHIRIKIANO

TANZANIA NA KOREA KUSINI WATIA SAINI MAENEO YA USHIRIKIANO

Katibu Mkuu Prof.Makubi akiwa na Viongozi kutoka KOFIH mara baada ya kutia saini maeneo ya mashirikiano baina ya nchi hizo mbili

Katibu Mkuu Prof.Makubi akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya KOFIH kutoka Korea ya Kusini Bw.Ha,Seung Rae(kushoto) na Naibu Mwakilishi Mkazi Bi.Kim Jungyoon(katikati) wakati wa kutia saini makubaliano ya mashirikiano Kati ya Wizara ya Afya na Taasisi hivyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof.Abel Makubi akiwa na Naibu Mwakilishi Mkazi kutoka Korea Foundation for International Healthcare(KOFIH),Bi.Kim Jungyoon Kwenye ofisi za Wizara zilizopo mji wa Serikali Mtumba.

DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya Prof.Abel Makubi, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Ha Seung Rae, Mwakilishi Mkazi  wa Taasisi ya Serikali ya Korea Kusini (Korea Foundation for International Healthcare-KOFIH) Kwenye ofisi za wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao pia wametia saini makubaliano mapya baina ya nchi hizo mbili Katika  maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo mafunzo na kuijengea uwezo maabara ya Taifa ya Jamii.

Prof. Makubi ameishukuru Taasisi hiyo kwa ushirikiano uliopo na kuendelea kuisaidia Serikali na ameahidi miradi yote itaendelezwa vizuri ili kuleta manufaa kwa nchi.

Hata hivyo Prof.Makubi ametumia muda huo kwa  kuwashukuru KOFIH kwa ushirikiano wao na Serikali Katika  kipindi Cha kukabiliana na janga la Corona mwaka jana.

KOFIH ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Afya nchini Korea Kusini ambapo inashirikiana na Wizara ya Afya Tanzania Katika maeneo ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya afya, Mradi wa kutoa ushauri, mafunzo kwa wataalam pamoja na mafunzo kwa upande wa injinia wa vifaa tiba.
Previous articleHALMASHAURI YA WILAYA MBINGA YAKABIDHI KIWANDA CHA MATOFALI KWA KIKUNDI CHA VIJANA
Next articleDKT.MPANGO ATEMBELEWA NA MKURUGENZI WA NCHI ZA AFRIKA BENKI YA DUNIA IKULU CHAMWINO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here