Home SPORTS STARTIMES NA K4S WAHAIDI KUBORESHA FURSA KWA VIJANA

STARTIMES NA K4S WAHAIDI KUBORESHA FURSA KWA VIJANA

DAR ES SALAAM.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi K4S Biko Scanda amehaidi kushirikiana na Kampuni ya Startimes kidhati ili kuhakikisha hali ya kiusalama zaidi katika Michezo.

Amebainisha hayo leo wakati akizungumza na wandishi wa habari katika uzinduzi wa chaneli ya TV 3 ambayo imeweka kipaombele katika maswala ya michezo.

“Kampuni yetu imekua miongoni mwa wadau wa michezo hasa Mchezo wa ngumi na kuhakikisha ulinzi una imarika zaidi tuna ungana na TV 3 katika kuimarisha na kukuza michezo hapa nchi kwa usalama wa hali ya juu,” anasema Biko.

Aliongeza  kuwa  Kampuni hiyo  imejitosa n
kuendelea kutoa fursa za ajira mbalimbali kwa vijana kwani kuna baadhi ya vijana wengi wanajiingiza kwenye vitu vinavyohatarisha maisha yao na kupelekea kuwa vibaka.

“Kupitia K4S pamoja na Startimes tunazingatia kuendelea kutoa fursa za ajira zaidi na tunategemea mechi ya ufunguzi wa Euro 2020 leo katika uwanja wa Zakhiem tutaimarisha ulinzi wa kutosha

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Clouds Media group Joseph Kusaga ambae ni mdau ea tasinia ya habari, amesema kutokana na michezo kupewa nafasi kubwa kwenye jamii inaonyesha iko wazi kuwa kupitia Sekta hiyo tunaweza kufungua milango mingi ya ajira mbalimbali.

“Tulianza kutoa frusa kwa wasanii na wanamitindo tukafanikiwa kuwafikia wengi na kutimiza ndoto zao sasa ni dhamu ya wanamichezo kuinuliwa kupitia TV 3 niwaombe kutumia frusa hii kwa upana ili kuinua tasnia hii” anasema  Kusaga. 

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kwa jinsi gani Startimes wanavoendelea kuboresha huduma zao kwa kuwapatia wateja wao vitu vizuri na vyenye kukata kiu kuanzia Michezo, Filamu pamoja na tamthilia kwa Lugha ya Kiswahili.

Tv3 kwa Sasa itatoa nyanja ya kutangaza vitu vilivyopo nchini kwetu Kimichezo na tamthilia hivyo itatupa fursa ya kutangaza utalii uliopo nchini kwetu hasa kukuza Lugha yetu ya Kiswahili.”
Previous articleWAZIRI WA FEDHA DKT. MWIGULU NCHEMBA AWASILISHA BAJETI KUU YA SERIKALI YA MWAKA 2021/2022
Next articleRC CHALAMILA ATENGULIWA, MHANDISI GABRIEL ACHUKUA NAFASI YAKE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here