Home LOCAL RC MAKALLA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA.

RC MAKALLA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA.

DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo June 21 amewaapisha Wakuu wapya wa Wilaya za Kigamboni na Ubungo walioteuliwa na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa Wiki.

Wakuu wa Wilaya walioapishwa na RC Makalla ni pamoja na Mhe. Kheri James* alieapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo pamoja na Mhe.Fatma Almass Nyangasa alieapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.

Akizungumza wakati wa kuwaapisha Viongozi hao RC Makalla amewataka Viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusimamia ukusanyaji wa Mapato, kushughulikia kero za Wananchi, ulinzi na usalama, Usafi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Previous articleWASHIRIKI MISS MWANZA WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM.
Next articleMAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWATAKA WATUMISHI WA MSD KUWA WAADILIFU NA KUACHA KUFANYA BIASHARA YA DAWA KWA MANUFAA YAO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here