Home ENTERTAINMENTS WASHIRIKI MISS MWANZA WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM.

WASHIRIKI MISS MWANZA WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM.

Na: MWANDISHI WETU.

WASHIRIKI  wa miss Mwanza 2021 na uongozi wao wametembelea kituo cha kulelea watoto wenyewe uhitaji maalum Hisani Center wilayani Ilemela  Buswera na kushiriki nao michezo mbalimbali.

Akizungumza wakati akikabidhi zawadi walizo enda nazo Mkurugenzi wa shindano hilo Sebastian Kaluguru, amesema moja ya kazi ya warembo ni kuwa karibu na jamii na kutoa huduma hausika kwa wale wanaohitaji.

“Leo tumekuja kutembelea watoto ambao wanaishi katika kituo hichi cha Hisani Center, pamoja na zawadi ambazo zitawasidi katika maisha yao ya hapa nyumbani hii itakuwa ni endelevu  tutatembelea vituo mbalimbali wakati hii wa kambi na baada ya kumaliza mashindano mshindi atakaye patikana ataendeleza mfumo huu,” anasema Kaluguru.

Aliongeza kuwa jamii haipaswi kuwasahau watoto wanaoishi katika mazingira magum hivyo ameomba mashirika, taasisi na serekali kuwa kumbuka mara kwa mara na kuunda kampeni pamoja na sera zitakazo wasaidi kujikwamua.

Kwa upande wa mlezi wa kituo hicho Grece Pita ameshukuru uongozi wa miss Mwanza na kuwakaribisha watu ambao wana uwezo wa kuwasaidi watoto hao kwa upande wa chakula, elimu na afya na ushauri kujitokeza.

“Nichukuwe nafasi hii kuiomba jamii kutembelea vituo hivi vya kulelea watoto kujua mahitaji yao, kuwashauri pamoja na kutenga muda wa kucheza nao ni faraja kubwa wanavyo ipata.”

Previous articleWAZIRI UMMY MWALIMU, LIBETALA MULAMULA WASISITIZA UMUHIMU WA KUTUNZA MAZINGIRA
Next articleRC MAKALLA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here