Home LOCAL MGANGA MKUU WA SERIKALI AHIMIZA WATUMISHI WA AFYA KUFANYA KAZI KWA BIDII

MGANGA MKUU WA SERIKALI AHIMIZA WATUMISHI WA AFYA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Na:WAMJW-Kibaha
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Aifelo Sichalwe amewataka watumishi wa sekta ya afya nchini kufanya kazi kwa bidii  ili kuweza kutimiza lengo la Serikali la kutoa matibabu bora na kwa wakati kwa wananchi wake.
Dkt.Sichalwe ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na watumishi wa afya wa hospitali ya Rufaa ya Tumbi mkoani Pwani mara baada ya kutembelea hospitalini hapo lengo ikiwa ni kukagua miundombinu na utayari wa  hospitali Katika kukabiliana na Magonjwa ya mlipuko ikiwemo Corona.
Dkt.Sichalwe amefikia hatua hiyo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais na Viongozi wa wizara ya afya katika kuhakikisha tahadhari ya kutosha inachukuliwa ili kuhakikisha Tanzania imejipanga kukabiliana  na wimbi la tatu la Virusi Vya Corona.
Ili kuendelea kujikinga na Magonjwa hayo Mganga Mkuu huyo aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha wanaweka vipukusi mkono(Sanitaizer) au Maji safi na Sabuni milangoni na kwenye mawodi sambamba na uvaaji wa Barakoa kwa kila aingiaye ndani ya hospitali.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt.Gunini Kamba alisema wameyapokea maagizo hayo kutoka serikalini na atahakikisha hatua za haraka zinaanza kuchukulia huku akimuhakikishia Mganga Mkuu wa Serikali kuendelea kusimamia nidhamu na maadili kwa watumishi ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya katika hospitali  hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here