Home Uncategorized KUMEKUCHA MISS DODOMA 2021.

KUMEKUCHA MISS DODOMA 2021.

NA: MWANDISHI WETU.

WALIMBWENDE  wanao wania taji la miss Dodoma mwaka huu wanatarajia kufanya shindano la vipaji June 19 katika hoteli ya Morena.

Warembo hao wote wataonyesha vipaji tofauti kuimba, kucheza, kuigiza , ubunifu na kuchora kisha watatangazwa watano waliofanya vizuri zaidi na mshindi atatangazwa katika kilele cha mashindano hayo.

Akizungumza na wandishi wa habari Mkurugenzi wa Nikalex Limited,  Alexandar Nikitas, ambaye ndie muandaaji wa shindano, amewaomba wadau mbalimbali na wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

“Napenda kuwa karibisha wadau wa mitindo na watu wote kujitokeza katika hotel ya Morena kushuhudia warembo wakichuana kuwania taji la ‘Miss Talent’ ambalo litatolewa siku ya fainali, ” anasema Alexander.

Aliongeza kuwa fainali za shindano hilo zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu katika hoteli ya Royo  Villlage mkoani humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here