Home LOCAL MAOFISA HABARI: USIMAMIZI SHIRIKISHI WA WADAU UTALINDA MAZINGIRA

MAOFISA HABARI: USIMAMIZI SHIRIKISHI WA WADAU UTALINDA MAZINGIRA

Emmanuel Lyimo Mkurugenzi Msaidizi Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG) akiongozana na Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakati walipotembelea baadhi ya madarasa ya shule ya msingi Kitunduweta yaliyojengwa kutokana na mradi huo katika kijiji hicho.

Kulangwa Ganga Katibu wa Wachoma Mkaa katika Kijiji cha Kitunduweta wilayani Kilosa akielezea namna wanavyochoma mkaa katika njia ya kisasa ambayo inawafanya kupata mkaa mwingi wakati maofisa habari na Mawasiliano Serikalini walipotembelea  Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) na dhana ya uendelevu wa misitu ya vijiji na kulinda mazingira nchini katika kijiji cha Kitunduweta wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.

Tanuri la Kisasa la kuchomea mkaa ambalo lnazalisha mkaa mwingi wakati wa kuchoma mkaa.

Charles Leonard Meneja Mradi wa kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania TTCS akiwaelezea maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini namna sekta hiyo ya Mkaa inavyoleta manufaa kwa wanavijiji seikali yenyewe na Halmashauri wakati walipotembelea na kujionea namna ya kuchoma tanuru la mkaa katika kijiji cha Kitunduweta wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.

Kutoka kulia ni Charles Leonard Meneja Mradi wa kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania TTCS, Emmanuel Lyimo Mkurugenzi Msaidizi Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG) na Mwandishi wa Habari kutoka Magazeti ya Serikali TSN Bw. Khamis Kibari wakiongoza maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakati walipotembele  mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) na dhana ya uendelevu wa misitu ya vijiji na kulinda mazingira nchini katika kijiji cha Kitunduweta wilayani Kilosa.

Charles Leonard Meneja Mradi wa kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania TTCS akizungumza viongozi wa kamati ya ulinzi wa misitu katika kijiji cha Kitunduweta Kilosa mkoani Morogoro. 

Emmanuel Lyimo Mkurugenzi Msaidizi Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG) akiongozana na Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakati walipotembelea baadhi ya madarasa ya shule ya msingi Kitunduweta yaliyojengwa kutokana na mradi huo katika kijiji hicho.

Emmanuel Lyimo Mkurugenzi Msaidizi Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG) akizingumza na Fred Kibano Afisa Habari OR- TAMISEMI wakati maofisa habari wa Serikali walipotembelea katika msitu wa Kitunduweta ambao mradi huo wa Mkaa Endelevu unatekelezwa katikati ni Elida Fundi kutoka Shirika la (MJUMITA).

Choo cha Mwalimu kilichojengwa kupitia mradi huo.

Kulangwa Ganga Katibu wa Wachoma Mkuu katika Kijiji cha Kitunduweta wilayani Kilosa akionesha nyumba ya mwalimu iliyojengwa katika kijiji hicho kutokana na utekekezaji wa mradi wa mkaa endelevu.

Thomas Lukoo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitunduweta akiwaelezea Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakati walipotembelea mradi wa mkaa endelevu katika kijiji hicho.

Leons Msoloka Katibu wa Kamati ya Maliasili katika kijiji cha Kitunduweta akielezea faida za misitu katika kijiji hicho.

John Mtimbanjayo Afisa Maliasili wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro akizungumza na Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakati walipotembelea kijiji cha Kitunduweta na kujionea shughuli za Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) na dhana ya uendelevu wa misitu ya vijiji na kulinda mazingira Nchini.

Na: Suleiman Msuya, Kilosa.
MAOFISA habari kutoka Serikalini na mashirika yasiyo ya Kiserikali wamesema Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) umetekeleza dhana ya uendelevu wa misitu ya vijiji na kulinda mazingira nchini.

TTCS ni Mradi unaotekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC).

Mradi huo unatekelezwa kwenye vijiji 30 vya wilaya ya Kilosa, Mvomero na Morogoro mkoani Morogoro ambapo umelenga Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ) wenye tija kwa jamii husika.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hii baada ya ziara ya siku moja kwenye Kijiji cha Kitunduweta wilayani Kilosa maofisa habari hao wamesema mradi huo unapaswa kuendelezwa nchini kote kwa sababu una manufaa kwa nchi na wananchi.

Fredick Bano Ofisa Mawasiliano Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amesema ziara hiyo amejifunza mambo mengi ambayo yanamatokeo chanya hivyo ameahidi kuelezea kwa viongozi wenzeka faida za TTCS.

Bano amesema TTCS imechochea utunzaji mazingira na kuinua kipato cha wananchi hivyo inapaswa kusambazwa katika vijiji vyote vyenye misitu ya asili inayofaa kwa shughuli kama zinazofanyika Kitunduweta.

“Ujumbe wangu kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu kuendelea kuwaasa viongozi wa halmashauri wa kisiasa na kiserikali kushirikiana na wananchi kutunza misitu na mazingira kwa njia endelevu,” amesema.

Ofisa huyo amesema kupitia mafanikio ambayo ameyaona Kitunduweta atatumia nafasi yake kushawishi uwepo wa bajeti ya kutosha kwenye USMJ.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa Wilaya ya Kilosa Gladis Mapeka amesema ziara hiyo imempatia mafunzo mazuri ya namna ya kutumia misitu kwa njia endelevu.

Mapeka amesema amejifunza namna ya kukata mkaa kwa njia endelevu hali ambayo inaendeleza uoto wa asili kwa siku zijazo.

“Mradi huu wa TTCS unapaswa kuendelezwa kwani unafaida za kimazingira, uchumi, huduma za jamii na maendeleo.

Mfano tumeambiwa kuwa kila mshiriki anapata kiasi fulani mfano tumeshuhudia ujenzi wa darasa, nyumba ya mwalimu, choo na hhduma nyingine muhimu,” amesema.

Meneja Masoko wa Shirika la Kuhifadhi Mpingo na Maendeleo (MCDI), Innocent Kalokola, amesema ziara hiyo imempatia manufaa mengi na kuomba isambae nchini kote.

Kalokola amesema dhana ya uhifadhi endelevu inayotekelezwa Kitunduweta inachochea misitu kuwa salama kwani miti michache inazalisha mkaa kidogo.

“Huu mradi unapaswa kusambaa. Niombe Serikali na wadau wengine wa kushiriki kuisambaza,” amesema.

Kalokola amesema kinachofanywa na TFCG na MJUMITA katika mradi wa TTCS kinashabihina na miradi ya MCDI pamoja na kutokuwepo na uchomaji mkaa.

Naye Ofisa Mazingira na Elimu wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati, Kawa Kafuru amesema shughuli za uhifadhi wa misiti Kitunduweta zina tija kwa jamii.

Kafuru amesema njia zinazotumika kuvuna misitu ni njia rafiki kwenye msitu jambo ambalo linaweza kusambazwa nchini.

“Wakati nakuja nilitarajia kuona jangwa lakini kiujumla msitu upo katika hali salama jambo ambalo linathibitisha dhana ya uendelevu,” amesema.

Akizungumzia dhamira ya kuwapeleka maofisa habari hao kutoka wizara na taasisi mbalimbali Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo amesema wanaamini maofisa hao watakuwa mabalozi wazuri kwa viongozi na ofisi zao.

Lyimo amesema TFCG na MJUMITA kupitia TTCS, wamefanikiwa kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu kulinda, kutunza na kutumia rasilimali misitu hivyo wangependa mabadiliko hayo yasambae kila kona ya nchi.

“Misitu ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya nchi ila inahitaji ushirikiano kuhakikisha inakuwa endelevu hivyo kupitia maofisa habari hawa dhana hii ya uendelevu itasambaa,” amesema.

Meneja Mradi wa TTCS, Charles Leonard amesema ili misitu iweze kuwa endelevu ni lazima jamii inayozunguka iweze kunufaika na mradi huo umeonesha matunda chanya.

“Tanzania ina hekta milioni 48.1 za misitu ambapo hekta milioni 22 ni misitu ya vijiji ila iliyopo kwenye USMJ ni hekta milioni 1.5 hivyo ni wazi nguvu zinahitajika kuhakikisha hekta zaidi ya milioni 20 zinahifadhiwa kwa njia endelevu,” amesema.

Meneja huyo amesema takwimu zinaonesha kwa  mwaka zaidi hekta 479,000 zinapotea hii ikiwa ni mkoa wa Dar es Salaam mara tatu hivyo ni vema serikali na wadau kuwekeza kwenye utunzaji na uhifadhi misitu kwa njia endelevu.
Previous articleMAGAZETI YA LEO J.TANO JUNI 16-2021
Next articleKUMEKUCHA MISS DODOMA 2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here