Bi Eugenia Mkumbo (kushoto) akipokea cheti cha mabadiliko ya usajili wa jina la biashara kutoka umiliki binafsi kwenda umiliki wa kampuni kutoka kwa Afisa Usajili Msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Maryglory Mmary (kulia), baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili katika banda la BRELA kwenye maonesho ya Biashara yanayofanyika katika kiwanja cha Mwahako jijini Tanga. Maonesho haya yaliyoanza Mei 28, 2021, yatahitimishwa rasmi Juni 6, 2021.