Mwanadiplomasia ya Shahada ya Juu Juliana Lubuva ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee Kata ya Kijichi .aliyekoshwa na Hatua ya Rais Samia kukutana na wazee mwishoni mwa wiki iliyopita |
Na: Mwandishi wetu.
MWANA DIPLOMASIA ya Shahada ya Juu ambaye pia ni Naibu katibu wa Baraza la wazee Kata ya Kijichi Juliana Lubuva amempongeza rais Samia Suluha Hassan kwa hatua yake ya kukutana na wazee na kupata fursa ya kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu ujenzi wa taifa.
Juliana Wamesema kuwa Rais Samia alichokifanya ni kitu kizuri sana kwani kitendo cha kukaa pamoja na wazee na kujadiliana baadhi ya mambo ni hatua kubwa na ya mfano kabisa na kikubwa amekuwa muwazi katika yale anayoyaamini kwenye serikali yake.
Akizungumza siku moja baada ya kikao hicho ambacho kilifanyika katika viwanja vya mlimani city Mkoani hapa Juliana alisema Rais Samia amefanya jambo kubwa na lakupongezwa na ameweza kufafanua mengi juu ya mstakabali wa wazee.
“Rais Samia ametutendea haki wazee wa Dar Es Salaam kwaniaba ya wengine hapa nchini kwani hata katika hotuba yake unaona kabisa kwamba anachokiongea kinatoka moyoni kwake na si vinginevyo” alisema
Nakuongeza kuwa “kuna haja kama taifa kurudi kwenye maadili kwani hivi sasa maadili yameporomoka sana na ndio maana leo hii kijana hawezi kumpisha Mzee kwenye vyombo vya usafiri Jambo ambalo huko nyuma halikuwepo.
Juliana amemuelezea Rais Samia kama mwanamama jasiri na Mwenye mitazamo chanya Kwa nchi yake na watu wake na ndio maana amekuwa mkweli hata kuelekea mabadiliko ambayo ametangaza kuyafanya ndani ya Serikali yake.
Alifafanua kuwa katika kikao hicho wazee walikuwa na mahitaji yao ambayo wanataka watimiziwe ikiwa pamoja na asilimia 10 zinazotokana na mapato ya Halmashauri na wao waweze kufikiriwa kwani ni sehemu ya kundi maalum .
Pia uwakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama vile Bunge na mamlaka zingine ili na wao waweze kuwa na mtu wakuwasemea changamoto zao, lakini pia kwenye sekta ya afya wamesema bado hakujakuwa rafiki sana Kwa upande wao.
“kiukweli Rais Samia ameonyesha kukubaliana na hoja karibu zote za wazee huku akihaidi kuzifanyia kazi siku za mbeleni na zingine tumemsikia akimwagiza Waziri wa afya kushughulikia haraka hususani kero zinazohusu afya.”alisema Juliana.
Juliana amesema kingine ambacho kilimvutia ni jinsi Rais alivyokuwa muazi ambapo amewaeleza wazee kuwa tayari na kuyapokea mabadiliko ambayo atayafanya siku si nyingi huku akisema anajua kuwa watoto wao wapo.lakini waweze wavumilivu.
Hata hivyo alisema rais Samia amewaeleza kwamba kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa katika nchi ndio maana hata suala la kupandisha mishahara litafanywa hapo baadae huku akisisitiza kumaliza miradi yote ya kimkakati.
Mwisho