Home ENTERTAINMENTS MISS DODOMA KUMENOGA.

MISS DODOMA KUMENOGA.

Na: MWANDISHI WETU.

Shindano la kumsaka mrembo atakaye wakilisha mkoa wa Dodoma katika kinyang’anyiro cha miss Tanzania mwaka huu limezinduliwa rasmi leo.

Mchuano huo unatarajiwa kufanyika June 21jijini Dodoma  ambapo warembo zaidi ya 20 watashindana katika jukwaa moja kutwaa taji hilo.

Akizungumza na waandishi  wa habari, mlezi wa shindano hilo Mbunge wa viti maalum Morogoro Norah Mzeru amesema tasnia ya urembo inahitaji kuungwa mkono kwa kuwa imekuwa ikiibua vipaji vya wasichana

“Nikiwa kama mbunge wa viti maalumu mkoa wa Morogoro katika Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania nawaomba wabunge wenzangu kuchangia tasnii ya urembo na mitindo kwani inatoa Ajira kwa mabinti zetu pamoja na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji na utalii hapa nchini,”anasema Norah Mzeru.

Kwa upande wake  mkurugenzi wa NIKALEX LTD Alexander Nikitas ambae ni mwandaaji wa mashindano haya  amesema kuwa hii ni fursa kwa mabinti wa mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi ili kushiriki mashindano haya ambayo yatawapa nafasi za kushiriki Miss Tanzania ambapo mshindi wa kwanza mpaka wa tatu ndiye atakayepata nafasi  ya kushiriki Miss Kanda Kati.

“Mashindano haya yanayotarajia kufanyika Tarehe 21 mwezi wa 6 mwaka huu yatahusisha wilaya zote saba za Dodoma hivyo mabinti wote mnakaribishwa kushiriki mashindano kwa kuchukua fomu katika mitandao ya kijamii ukurasa za Miss Tanzania,”amesema Alexander Nikitas.

Pia Alexander Nikitas amesema jamii itambue kuwa tasnia ya urembo na mitindo  imekuwa chachu katika kuwajengea mabinti kuwa wana jamii wenye kutegemewa kwa kuanzisha kampeni za kusaidia na kuelimisha jamii katika sekta mbalimbali

Previous articleMWANA DIPLOMASIA YA SHAHADA YA JUU JULIANA LUBUVA AMPONGEZA RAIS SAMIA.
Next articleHALMASHAURI YA MALINYI KUWAKAMATA WAVAMIZI BONDE LA MAJI LA MWALIMU NYERERE.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here