Home ENTERTAINMENTS DKT.ABBASI:MIFUMO YA HAKIMILIKI KULINDA MASLAHI YA KAZI ZA SANAA

DKT.ABBASI:MIFUMO YA HAKIMILIKI KULINDA MASLAHI YA KAZI ZA SANAA

 

 
Na: Mwandishi Wetu.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema  Serikali inaweka Mifumo bora kwa ajili ya kuboresha kazi za sanaa na kulinda masalahi ya Wasanii.
 

Dkt. Abbasi ameyasema hayo Mei 9, 2021 kwenye Iftar maalum iliyoandaliwa na Star Times kuzindua tamthilia mpya ya WE-MEN na Chaneli mpya ya TV3 katika Ukumbi wa Hyatti jijini Dar es salaam.
 

“Kazi za Wasanii wengi wa hapa nchini zinachezwa na kuangaliwa sana duniani lakini wamiliki wa kazi hizo hampati chochote” amesema Dkt. Abbasi.
 

Dkt. Abbasi amefafanua kuwa kupitia mwaka mpya wa fedha wa 2021/22  Serikali itakua na  kodi maalumu ya kutoza makampuni mbalimbali  yanayokuja nchini kwa ajili ya  kutumia ama kuuza kazi za wasanii ambayo  itamfaidisha msanii moja kwa moja.
 

Aidha  Katibu Mkuu Dkt.Abbasi amewasisitiza wasanii kufanya kazi bora kwasabau muziki, filamu na sanaa zima kwa ujumla duniani ipo katika ushindani mkubwa, hivyo wanapaswa kutengeneza kazi zenye kiwango cha hali ya juu kukidhi mahitaji na Soko Duniani.
 

Hata hivyo Dkt. Abbasi ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuwekeza katika filamu za kitanzania na pia kwa kuanzisha Chaneli mpya ya TV3 itakayokuwa inarusha mashindano ya EURO 2020 ambayo uchambuzi  wa mashindano hayo utakuwa ukifanyika kwa lugha ya kiswahili.
 

“Nawashukuru Star Times kwa kazi kubwa mnayoifanya Tanzania, mmetafuta soko la kazi zetu za sanaa hongereni sana” Dkt. Abbasi.
 

Awali  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiago kilonzo amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la watazamaji wa tamthilia zetu za kitanzania na hii si kwa Tanzania peke yake, bali hata nchi za jirani kama vile Kenye na Uganda wanafuatilia sana tamthilia za hapa nchini, Hii ni ishara kwamba tamthilia zetu zinafanya vizuri kimataifa.
 

Dkt. Kilonzo ameongeza kuwa  tamthilia hiyo itatoa takriban ajira 100 kwenye Sekta ya Sanaa hapa nchini

Previous articleBENKI YA NMB YADHAMINI MASHINDANO YA KITAIFA YA SAYANSI,TEKNOLOJIA NA UBUNIFU
Next articleMWANA DIPLOMASIA YA SHAHADA YA JUU JULIANA LUBUVA AMPONGEZA RAIS SAMIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here