Home SPORTS MAJALIWA AZUNGUMZIA SAKATA LA MECHI YA SIMBA NA YANGA, BUNGENI

MAJALIWA AZUNGUMZIA SAKATA LA MECHI YA SIMBA NA YANGA, BUNGENI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  Bungeni jijini Dodoma kuhusu maagizo ambayo ameyatoa kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, juu ya sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Simba na Yanga ambayo ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa  Dar es salaam, Mei 8, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na.Alex Sonna,DODOMA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesimama bungeni kuzungumzia tukio la kuahirishwa kwa mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga uliokuwa uchezwe Jumamosi, tarehe 8/05/2021.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa haraka sana kwa Watanzania juu ya tarehe ya kuchezwa kwa mchezo huo na pia ieleze utaratibu kuhusu hatima ya waliolipa viingilio ili kushuhudia mchezo huo.

”Niwasihi Watanzania  kuwa wavumulivu ili kuipa muda Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia mpira wa miguu ikiwemo TFF kuja na taarifa juu ya hatima ya mchezo huo”amesema 

Mchezo wa Simba na Yanga ulipangwa kufanyika Mei 8,2021katika uwanja wa Benjamin Mkapa  uliahirishwa kutokana na mabadiliko ya muda wa awali ambao ulipangwa kuwa saa 11:00 jioni lakini kabla muda huo kufika, TFF litoa taarifa ya kubadili muda mpaka saa 1:00 usiku.

Previous articleIGP SIRRO AKUTANA NA IGP WA NCHI YA RWANDA
Next articleBENKI YA NMB YADHAMINI MASHINDANO YA KITAIFA YA SAYANSI,TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here