Home FASHIONS KAMPUNI YA SEMS APPAREL KUGUSA WENYE MAHITAJI

KAMPUNI YA SEMS APPAREL KUGUSA WENYE MAHITAJI


Na. MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Sems Apparel limited, pamoja na wadau wa mitindo Ety’screation wameandaa  harambe ya kuchangia watu wenye mahitaji maalum katika jamii.
Harambee hiyo itafanyika Mei 8 Osterbay Msasani, kwa kushiriki katika Iftari ambayo itafwatiwa na onyesho la mavazi kutoka kwa wabunifu wa Sems Appael Limited.
Akizungumza na Mtanzania Digital, mratibu ya shuhuli hiyo Sammy Diwani ‘Etyscreations,’ amesema wameadhimia kukusanya fedha ambazo zitakabidhiwa kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshuhulikia Wenya Ulemavu Ummy Nderiananga, kawa ajili ya kununua vifaa vya watu wenyewe ulemavu.
“Tutakuwa na Ifutari ya pamoja, baada ya hapo kutafanyika onyesho la mavazi ambayo yatanadiwa na kuuzwa kwa ajili ya kupata fedha za kusaidia watu wasio jiweza,” anasema Etyscreation.
Pia katika shuhuli hiyo itahudhuriwa na mgeni rasmi kutoka katika ofisi ya  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshuhulikia Wenya Ulemavu ambaye atamuwakilisha Mheshimiwa Ummy Nderiananga.
Aliongeza kuwa wana karibisha watu wote kushiriki katika changizo hilo kwa kununua kadi shilingi 50000 kupitia mtandao wa  Nilipe app.
Previous articleMISS PWANI YAKARIBISHA WADHAMINI.
Next articleTUTASIMAMA NA WAKUNGA KUHAKIKISHA UZAZI UNAKUWA BARAKA, FURAHA TANZANIA – DK GWAJIMA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here