Home BUSINESS JAMII YAKUMBUSHWA UMUHIMU WA KUWA NA BIMA KATIKA NYANJA MBALIMBALI.

JAMII YAKUMBUSHWA UMUHIMU WA KUWA NA BIMA KATIKA NYANJA MBALIMBALI.

Afisa Mtendaji mkuu wa Sanlam Life insurance limeted & Sanlam general insurance, wa katikati Bwana Julius Magabe akiongea na waandishi wa habari.

Na Richard Mrusha

Wito umetolewa kwa jamii kujiunga na huduma za  Bima mbalimbali kwani zinaumuhimu mkubwa Sana kwa mustakabali wa Maisha yao ya kila siku.

Wito huo umetolewa na Afisa  Mtendaji mkuu wa Sanlam Life Insurance Tanzania Limited & Sanlam general insurance,na  Mkurengezi wa kanda ya  Afrika Mashariki, Julius Magabe amesema kuwa huduma za Bima zina mustakabali mkubwa kwa Taifa,uchumi wake na jamii kwa ujumla.

Amesema Kwani kinga zitolewazo na kampuni za Bima husaidia mlaji wa huduma kujikinga na athari za kiuchumi zitokanazo na majanga mbalimbali ikiwemo moto,mafuriko,wizi,ajali,ulemavu na hata vifo,lakini  pia kuweka akiba kwa ajili ya mipango ya baadae.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaaam wakati wakitambulisha kauli mbiu isemayo ishi kwa kujiamini.

Amesema pia humsaidia mlaji kujiamini ambayo ni hisia ya amani kuwa kile ambacho ni cha muhimu kwa jamii kinalindwa na mtu kuweza kuwa na amani moyoni kuwa anaweza kuendelea na kufikia kutimiza ndoto yake au malengo yake kwa kuwa yale aliyoyafikia yanaulinzi na kinga.

Amesema wao Kama sanlam wanajivunia sana kuwa sehemu ya utoaji wa kinga hii Muhimu nchini Tanzania na kuitaka jamii kujiunga na Bima hii ya Sanlam ili kuwa miongoni mwa watu wanaojiamini.

Previous articleWACHIMBAJI WADOGO WANAMCHANGO MKUBWA WA KUKUZA UCHUMI WA TANZANIA.
Next articleMTANANGE WA SIMBA NA YANGA WASOGEZWA MBELE SASA KUPIGWA SAA 1:00 USIKU.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here