Home SPORTS CAF YAIPIGA YANGA FAINI

CAF YAIPIGA YANGA FAINI


Na: Mwandishi wetu.

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeipiga faini ya Sh11 milioni klabu ya Yanga baada ya kushindwa kujibu madai ya kuwafanyia fujo baadhi ya watu waliokuwa kwenye msafara wa Rivers United ya Nigeria.

Malalamiko hayo yametokana na mechi ya hatua ya awali iliyochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Septemba 12 na Yanga kupoteza kwa bao 1-0, ambapo kupitia mitandao ya kijamii ya timu hiyo walilalamika kupigwa kwa watu mbalimbali akiwemo Ofisa habari wa timu hiyo, Charles Mayuku.

Rivers United walipeleka malalamiko hayo CAF na kupitia mtandao wao wamethibitisha kupokea malalamiko hayo.

Pia CAF wamesema mechi hiyo haikutakiwa kuwepo mashabiki ila walibaini baadhi ya mashabiki uwanjani.

CAF ilituma malalamiko hayo kwa Yanga kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), na wamesema hakukuwa na mrejesho wowote kutoka kwenye Shirikisho hilo.

Kutokana na hilo bodi ya nidhamu imeipiga faini Yanga  kiasi cha  5,000 USD sawa na Sh11 milioni za kitanzania.

Previous articleKANISA ANGLIKANA TANZANIA DAYOSISI YA RUVUMA LAOMBA SERIKALI KUITAZAMA HOSPITALI YA MT. ANNA LIULI.
Next articleMAGAZETI YA LEO J.TANO OCTOBA 13-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here