MWENGE WA UHURU WATUA KWENYE KIWANDA CHA BIA CHA GAKI SHINYANGA
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akitembelea Kiwanda cha Bia Gaki Investment Co. Ltd.Na Marco Maduhu, SHINYANGA KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma amewasili katika Kiwanda cha Bia Gaki Investment Co. LTD na kuweka Jiwe la Msingi, na kupongeza kwa uwekezaji mkubwa ambao utatatua changamoto ya Ajira kwa Vijana...
NAIBU WAZIRI MASANJA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA MPYA 400 MSOMERA WILAYANI HANDENI
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekagua ujenzi wa nyumba mpya 400 katika kijiji cha Msomera Wilayani Handeni, Mkoani Tanga watakazohamia kwa hiari wananchi kutoka Ngorongoro.Akizungumza leo katika ziara hiyo, Mhe. Masanja amewapongeza SUMA JKT kwa kufanya kazi vizuri kuhakikisha nyumba hizo zinakamilika kwa wakati.“Maelekezo yetu ni kwamba hadi kufikia tarehe 30 Agosti 2022 kaya...
WATAALAMU KUTOKA NCHI ZINAZOZALISHA ALMASI AFRIKA ZASHUHUDIA MAFUNZO TGC
Wataalamu kutoka Nchi zinazozalisha Madini ya Almasi Afrika (ADPA) wamefurahishwa na mfumo wa mafunzo yanatolewa na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).Wataalamu hao, wamekitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha baada ya kufika jijini humo kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa Tatu wa ADPA unaoanza tarehe 28 Julai.Naye, Maurice Miema kutoka Jamhuri ya Kimokrasia ya Kongo amesema Tanzania imepiga hatua kubwa...
TANESCO SINGIDA YASAKA MAONI YA WANANCHI KUHUSU NISHATI YA UMEME
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida, Mhandisi Florence Mwakasege akizungumza na Wananchi wa Kata ya Iguguno wilayani Mkalama leo Julai 26, 2022 wakati akisikiliza mahitaji na ushauri wao kuhusu sekta ya nishati.Afisa Mtendaji Kata ya Iguguno, Josia Pangazi akizungumza kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Meneja wa Tanesco Wilaya ya Mkalama, Mhandisi, Benedict Ryeimamu, Meneja wa...
SERIKALI YA BRAZIL, WADAU KUWAONGEZEA NGUVU WAKULIMA WA PAMBA MWANZA
Na: Paul Zahoro, Mwanza RSMkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ametoa rai kwa wadau wa Kilimo Mkoani Mwanza kuunga mkono jitihada zinazolenga kuboresha uzalishaji wa zao la pamba ili kuongeza kipato kwa wananchi kwani ndio zao kuu la biashara Mkoani humo.Amesema hayo leo Julai 27, 2022 katika kikao kilichofanyika kwenye Hoteli ya Gold Crest mjini humo...
MAFUNDI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA ILEMELA KUJENGA KWA NUSUBEI KUUNGA MKONO KAMPENI
Na:Paul Zahoro, Mwanza RSShule ya Msingi Kahama wilayani Ilemela imepokea kijiti cha kampeni ya Mkoa ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni siku ya tatu tangu ilipoanza ambapo wananchi wamechimba Msingi wa vyumba vya Madarasa 9 katika kukabiliana na msongamano kwenye shule hiyo unaosababishwa na upungufu wa vyumba 38.Akiongoza kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi...