NA: MWANDISHI WETU.
MKURUGENZI wa bank ya Maendeleo Ibrahim Mwangalaba, amezindua msimu wa tano wa maonyesho ya Adorabo Wedding Trade Fair, katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar Es Salaam.
Onyesho hilo ambalo hufanyika kila mwaka na kutoa frusa kwa watoa huduma katika shuhuli mbalimbli kukutana na wateja kwa ajili ya kutanua wigo wa biashara limeanza rasm jana litadum mpaka Mei 15.
Akizungumza na wajasiria mali hao Mkurugenzi Ibrahim Mwangalaba, amewambia watoa huduma hao wajifinze kuwa na ampangilio mzuri wa mapato katika kazi zao.
“Tunatakiwa kuwa na utaratibu wa kuweka rekodi ili inapofika mwisho wa mwaka unafaham umepata faida kiasi gani hii itakusaidia kufahamu biashara yako inakua kwa kiasi gani hata unapohitaji mkopo inakua ni rahisi,” anasema Ibrahim Mwangalaba
Kabla ya uzinduzi huo Mkurugenzi huyo alipata nafasi ya kutembelea banda moja moja na kuongea na wajasiria mali hao ambapo aliwapatia ushauri kila mmoja kutokana na biashara yake.
Aidha aliwakatibisha katika kujiunga katika Bank ya Maendeleo kwa ajili ya kupata mikopo itakayo wakwamua katika biashara zao.
Kwa upande wa muasisi wa onyesho hilo Anna Lema alimshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuja kuzungumza na wajasiria mali na kuahidi kufanyia kazi ushauri alio wapatia.
Mbali na maonyesho hayo kutakuwa na bahati na sibu itakayo chezeshwa siku ya kilele cha tamasha hili kwa wana ndoa watarajiwa na washindi watapata zawadi ya kufanyiwa harusi yao kwa asilimia 80 na watoa huduma hao.