Home LOCAL RAIS SAMIA AKUBALI ONGEZEKO LA MSHAHARA KWA KIMA CHA CHINI KWA ASILIMIA...

RAIS SAMIA AKUBALI ONGEZEKO LA MSHAHARA KWA KIMA CHA CHINI KWA ASILIMIA 23.3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa 23.3%.

Mapendekezo hayo yaliyowasilishwa Ikulu ni mwendelezo wa kikao cha Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichofanya hivi karibuni mkoani Dodoma na kupokea taarifa ya wataalamu kuhusu nyongeza ya mishahara.

Nyongeza hiyo imefanyika kwa kuzingatia Pato la Taifa (GDP), mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa katika mwaka 2022/2023 na hali ya uchumi wa ndani na nje ya nchi.

Kutokana na hatua hiyo katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imepanga kutumia kiasi cha Shilingi trilioni 9.7 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.

Hivyo bajeti ya mishahara ya mwaka 2022/23 ina ongezeko la Shilingi trilioni 1.59 sawa na 19.51% ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22. 

Wakati huo huo, Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya Mafao ya Pensheni kama Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) lilivyoomba Mei mosi, 2022.

Mhe. Rais Samia ameridhia na kuielekeza wizara yenye dhamana na masuala ya hifadhi ya jamii kuendelea kushirikiana na TUCTA na Chama cha Waajiri nchini (ATE) ili kukamilisha taratibu za kuhakikisha malipo ya mkupuo ya 25% yaliokataliwa na wadau mwaka 2018 yanapandishwa hadi 33%.

Previous articleMSIMU WA TANO WA ADORABO WEDDING TRADE FAIR WAZINDULIWA
Next articleJESHI LA POLISI RUVUMA NA TAWA WAKAMATA MENO TEMBO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here