Home BUSINESS BoT HARAKISHENI MCHAKATO WA UNUNUZI WA DHAHABU: DKT. KIJAJI

BoT HARAKISHENI MCHAKATO WA UNUNUZI WA DHAHABU: DKT. KIJAJI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja wa Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Vick Msina (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo wakati alipotembelea Banda la  Taasisi  hiyo kwenye Maonesho ya 5 ya teknolojia ya Madini yaliyofungwa leo Oktoba 8,2022  kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita ambpo Dkt. Kijaji alikuwa mgeni rasmi. (wa kwanza kulia), ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela, na (wa tatu kulia), ni Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa kwanza kulia) akimsikiliza Meneja Msadizi Akiba ya Fedha za Kigeni wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Anna Lyimo (wa kwanza kushoto) alipokuwa akitoa maelezo wakati alipotembelea banda la  Benki hiyo kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya Madini yaliyofungwa leo mkoani Geita. (wa pili kulia), ni Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko, na (wa pili kuhoto), Meneja wa Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Vick Msina.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akizungumza na Meneja Msadizi Akiba ya Fedha za Kigeni wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Anna Lyimo (kushoto) kuhusu mchakato wa Benki hiyo kuanza kununua Dhahabu. (wa pili kulia), ni  Meneja wa Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Vick Msina akisikiliza mazungumzo ya Waziri Dkt. Kijajia alipotembelea banda la  Taasisi hiyo kwenye maonesho ya 5 ya teknolojia ya Madini yaliyofungwa rasmi leo Oktoba 8,2022 kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji  (wa tatu kushoto) akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa pili kwa Taasisi za kifedha Mkurugenzi wa BoT tawi la Mwanza Dkt. James Machemba baada ya benki hiyo kushinda katika maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini yaliyomalizika leo kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita. 

Meneja wa Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Vick Msina (kulia) akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano kwa Umma wa Benki hiyo Bi. Graciana Mahega (kushoto).

Meneja wa Idara ya Mawasiliano  Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Bi. Vick Msina akijadiliana jambo na Katibu Tawala wa mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara alipotembelea banda la BoT.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ameitaka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuharakisha mchakato wa kuanza kununua Dhahabu kabla ya kumalizika kwa mwaka huu ili kuwawezesha wachimbaji wakubwa na wachimaji wadogo kupata soko la uhakika.

Waziri Dkt. Kijaji ameyasema hayo leo Oktoba 8,2022 alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini yaliyofungwa leo kwenye viwanja vya EPZA Bombambili Mkoani Geita, ambapo Waziri Kijaji alikuwa Mgeni rasmi.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Meneja Msadizi Akiba ya Fedha za Kigeni wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Anna Lyimo, kuhusu mpango wa Taasisi hiyo kuanza kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji hapa nchini.

Dkt. Lyimo  ameelezea dhamira ya BoT na wajibu wa kisheria wa kuhifadhi akiba ya fedha za kigeni hapa nchini.

“Benki kuu imefanya tafiti mbalimbali kupata vyanzo ili kuongeza akiba ya fedha za kigeni, ambapo moja ya tafiti iliyofanywa baada ya mabadiliko na maboresho katika sheria ya madini na sekta ya madini kwa ujumla ni uanzishwaji wa viwanda vya kuchenjulia dhahabu, pamoja na kukua kwa teknolojia ya kupima viwango vya dhahabu ambavyo vyote kwa pamoja vimesaidia kuongeza kiwango cha fedha za kigeni hapa nchini” ameeleza Dkt. Lyimo.

Ameongeza kwamba madini hayo yatanunuliwa hapa nchini kwa fedha za kitanzania na baadae kupelekwa nje ili kuongezewa thamani ili yaweze kuthibitishwa katika viwango vya kimataifa na kuhifadhiwa katika masoko ya kimataifa kwa kutumia fedha zetu za kigeni zilizopo nchi za nje .

Aidha amezitaja faida mbalimbali zitakazopatikana kwa kununua dhahabu nchini ikiwa ni kuongeza kiwango cha akiba ya fedha za kigeni kwa bei nafuu, pamoja na kuisaidia serikali kupunguza kiwango cha mikopo ambayo serikali ingetakiwa kukopa ili kuongeza akiba ya fedha za kigeni.

Faida nyingine ni kuipatia sekta ya madini soko la uhakika ambapo wachimbaji wadogo na wakubwa wa madini badala ya kwenda kuuza madini yao katika masoko ya nje wanaweza kwenda BoT kuuza madini yao kwa bei nzuri na ya uhakika ambapo itawapunguzia gharama za kwenda nje ya nchi.

Amehitimisha kwa kusema Benki kuu itatoa taarifa kwa wananchi kuhusu tarehe rasmi ya kuanza kununua madini ya dhahabu nchini.

Previous articleMCHANGO WA SEKTA YA MADINI WAZIDI KUIMARIKA: DKT. KIJAJI
Next articleMNYAMA SIMBA KUUNGURUMA ANGOLA LEO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here