Home BUSINESS MBIBO AUNGA MKONO JUHUDI ZA STAMICO

MBIBO AUNGA MKONO JUHUDI ZA STAMICO

*Shigella atoa Ofa kwa wawekezaji kumi wa mwanzo*

Na: Mwandishi wetu, GEITA 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kununua mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe unaotekelezwa na Shirika hilo.

Mbibo amenunua mkaa huo baada ya kushiriki katika Siku ya Geita iliyotanguliwa na kongamano la uwekezaji na baadaye kutembelea banda la STAMICO katika Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini.

Aidha, Mbibo ametoa wito kwa STAMICO kuendelea kuutangaza mkaa huo ili wananchi waweze kuutambua na kuutumia kwa lengo la kuepusha ukataji wa miti na uharibifu wa mazingira.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella amezindua Jarida maalumu linaloangazia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ndani ya mkoa wa Geita.

Sambamba na hayo, Shigella amewaomba wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo mkoani humo ambapo ametoa ofa kwa wawekezaji kumi wa mwanzo watapatiwa eneo la kuwekeza bila malipo.

Maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yanatarajiwa kufungwa Oktoba 08, 2022.

Previous articleTAMASHA LA JINSIA KANDA YA KASKAZINI LAFUNGWA SAME..DC MPOGOLO ATAKA SHERIA ZITUMIKE KUMALIZA UKATILI WA KIJINSIA
Next articleBoT KUANZA KUNUNUA DHAHABU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here