Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kulia) akizungumza na Watumishi wa Mgodi wa uchimbaji wa dhahabu wa BUCKREEF alipofika katika banda lao kujionea shughuli wanazofanya katika Maonesho ya tano ya Sekta ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili EPZA Mkoani Geita.
Katika Maonesho hayo yanayotarajiwa kufikia tamati Oktoba 8,2022, Waziri Jaffo amekuwa mgeni rasmi katika siku ya leo Oktoba 6,2022 ambapo kabla ya kuanza ziara yake alipanda miti katika viwanja hivyo na kuipongeza BUCKREEF kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda jumla ya miti 6000 katika Mkoa wa Geita.
Hata hivyo aliitaka Kampuni hiyo kuendelea na upandaji miti katika maeneo mengine ikiwemo Mashuleni na katika maeneo mengine zinazotoa huduma za kijamii.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO – GEITA)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kulia) akizungumza na Watumishi wa Mgodi wa uchimbaji wa dhahabu wa BUCKREEF katika maonesho hayo. (wa kwanza kushoto) ni Meneja Rasirilimali watu wa BUCKREEF Amelda Msuya, (wa pili kushoto) ni, Mjiolojia wa Kampuni hiyo Jamal Makishe, (wa tatu) ni Afisa Rasirimali watu Domitilla Damas na (wa nne kushoto) ni, Mtaalamu wa Umeme wa BUCKREEF, Nahum Estomih.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Rasirimali watu wa BUCKREEF Domitilla Damas (kushoto) mara baada ya kumaliza ziara yake fupi katika Banda la Kampuni hiyo.