Home LOCAL RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA TAASISI...

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA TAASISI MBALIMBALI ZA DOHA NCHINI QATAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari pamoja na ujumbe wake, Doha nchini humo tarehe 06 Oktoba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania (iliowakilishwa na Rais wake Paul Koyi), Zanzibar (iliyowakilishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour pamoja na Chemba ya Biashara ya Qatar iliyowakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari.

Hafla ya utiaji saini wa Mkataba huo umefanyika Doha nchini Qatar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia makabidhiano mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania na Chemba ya Biashara ya Qatar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari mara baada ya mazungumzo, Doha nchini Qatar tarehe 06 Oktoba, 2022. Kushoto ni Rais wa Chemba ya Biashara ya Tanzania (TCCIA) Paul Koyi na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour.

Previous articleASHIRIKI SIKU YA PILI YA MKUTANO WA UBUNIFU WA AFYA DUNIANI DOHA NCHINI QATAR
Next articleWAZIRI JAFFO AIPONGEZA BUCKREEF KUPANDA MITI KATIKA VIJIJI VINAVYOZUNGUUKA MGODI HUO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here