NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Taasisi ya fedha ya CRDB imefanikiwa kupunguza asilimia sita ya mikopo chechefu kutoka kutoka asilimia 9 Hadi kufikia 3 kwa mwaka 2019-2022.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Abdulmajid Nseleka wakati akiongea waandishi wa habari jijini Arusha katika kuelekea mkutano mkuu wa 27 ya wanahisa wa Benki hiyo, ambapo alisesema kuwa kupitia mafanikio hayo pia wamefanikiwa kupunguza riba kwa kuangalia sekta muhimu inayoleta tija kubwa kwenye uchumi wa nchi ambayo ni kilimo.
“Lengo ni kugusa watu wengi walio kwenye sekta nzima ya kilimo ambapo wakulima wengi watafaidika na huduma wanazotoa benki ya CRDB kwa kununuliwa pembejeo au vitendea kazi mbalimbali na sekta ya pili kunufaika ni pamoja na wafanyakazi ambao tumewapunguzia riba kutoka asilimia 18 hadi 13 huku wanawake wajasiriamali wakipunguziwa kutoka asilimia 20 hadi 12,” Alisema Nsekela.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi CRDB,Ally Laay alieleza kuwa wamekuwa wakiwekeza elimu kwa wateja wao ikiwemo wanahisa ambao wapo zaidi ya laki sita ili kusaidia kuelewa umuhimu wa kuwekeza na namna ya kutumia fursa zinazojitokeza katika Benki ya CRDB lengo likiwa ni kumfikia Mwananchi mzawa nakutumia fursa zilizo
Naye Mkurugenzi wa mawasiliano, Tully ester Mwampamba aliwataka wanahisa kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura katika mtandao wao kuwachagua Wajumbe wa bodi ya wanahisa kuanzia Mei 18,2022.