Home SPORTS AZAM FC YAIKABA SIMBA CHAMAZI

AZAM FC YAIKABA SIMBA CHAMAZI

MABINGWA Watetezi Simba wameshindwa kutamba ugenini dhidi ya Azam FC baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Chamazi Complex nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Azam FC walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Simba katika dakika ya 17 bao likifungwa na Mshambuliajia Rodgers Kola,Mshambuliaji wa zamani wa Azam ,John Bocco aliisawazishia timu yake dakika ya 44.

Kipindi cha pili timu zote ziliafanya mabadiliko na kuanza kushambualiana kwa zamu hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zimeweze kugawa pointi moja moja.

Kwa Matokeo hayo Simba wamefikisha Pointi 50 wakizidiwa Pointi 10 na Vinara wa Ligi hiyo Yanga wenye Pointi 60 ,Timu zote zikiwa zimecheza mechi 24 na kubakiwa na mechi sita huku Azam FC wakibaki nafasi ya tano wakiwa na Pointi 33.

Previous articleUMMY MWALIMU: WANANCHI MSIAMINI TAARIFA ZA UPOTOSHAJI
Next articleUFARANSA KUFANYA UWEKEZAJI WA DOLA BILIONI 4.2 NCHINI TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here